Monday, October 18

Lewis Hamilton: Mwanamuziki aliyejikita kwenye mbio za magari.

Ni wanamichezo ambao uwezo,talanta na rekodi zao zitasalia katika kumbukumbu za historia kwa muda mrefu .Wengine wameshastaafu lakini wenzao bado wapo katika tasnia ya michezo.Wikii hii tunakupakulia safari za wanamichezo wa kipekee ambao wameng’ara na kuacha mifano ya kuigwa katika aina mbali mbali ya michezo.Leo tunamuangazia Dereva wa mashindano ya Formula 1 Lewis Hamilton

bbc

Ni dhahiri unaweza usijue sana kuhusu mbio za magari ya Formula 1, lakini utakuwa unamjua ama umewahi kulisikia jina la Lewis Hamilton.

Kila mchezo una magwiji wake, Hamilton ni gwiji wa mbio za magari ya’langalanga’ au formula 1 akiwa kundi moja la juu la magwiji wa michezo mingine mbalimbali duniani kama Michael Jordan, LeBron James (kikapu) Edson Pele, Diego Maradona, Cristiano Ronaldo na Messi (soka) na Mohamed Ally, Floyd Maywheather Jr na Mike Tyson (Masumbwi).

Hamilton ameifikia rekodi ya gwiji mwingine wa mbio hizo za magari ambazo ni za kasi na ghali, Michael Schumacher ya kushinda mara 91 kwenye ‘Grand prix’.

 

h

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Unaweza kumtaja kama gwiji wa mbio za magari na mwanamichezo mwenye mafanikio makubwa kutoka Uingereza, lakini nyuma ya pazia ni msanii wa muziki, mwanaharakati na mpenda mitindo asiyeficha moyo wake.

Lewis Hamilton ni nani?

Lewis

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lewis Hamilton akipongezwa na baba yake Anthony Hamilto, baada ya kuvunja rekodi yake ya kushinda mara 92 kwenye F1 Grand Prix iliyofanyika Ureno kwa jana.

Jina lake kamili ni Lewis Carl Davidson Hamilton akizaliwa Januari 7, 1985 huko Hertfordshire, England.

Ni mtoto pekee katika familia ya Anthony Hamilton, Muingereza mweusi na Carmen Larbalestier, mzungu. Kwa ufupi Hamilton amechanganya rangi lakini mwenyewe anajitambulisha kama mtu mweusi.

Akiwa na miaka miwili, wazazi wake walitengana, hivyo Hamilton alibaki kulelewa na mama pekee. Aliishi na mama yake pamoja na dada zake wa kufikia.

Kuna wakati akiwa na umri mdogo wa miaka 5, Hamilton alilazimika kujifunza Karate ili kujilinda mwenyewe na watoto wenzake waliokuwa wanamtania.

Walimtania kwa rangi yake, kwa kutokua na baba na kimo chake kilichoonekana kidogo.

Wapo ndugu waliodhani Hamilton angekuwa mcheza karate maarufu lakini mambo yalibadilika.

Lewis Hamilton na hadithi yake ya kuingia McLaren

British Go Kart

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Hamilton akiwa na umri wa miaka 12, akishangilia moja ya mbio za British Go Kart alizoshinda dhidi ya watoto wenzake

Tangu akiwa mtoto kabisa alionyesha wazi mapenzi yake kwenye michezo kadhaa, ukiacha karate, soka kiasi, lakini mapenzi yalijiegemeza zaidi kwenye michezo ya magari akianza kushindana kuendesha magari ya kitoto na watoto wenzie.

Hilo likamvutia Ron Dennis, ambaye alimuingiza kwenye mpango wa madereva makinda wa McLaren , hiyo ilikuwa mwaka 1998, akianza kufanya mazoezi na kupewa ujuzi wa kuendesha magari ya mashindano.

Akiwa na miaka 8 tu Hamilton alishaonyesha yeye ni mkali akishinda mbio za magari za shuleni. Akiwa na miaka 10, Hamilton alikutana na Ron Dennis, Bosi wa McLaren akamuomba amsainie kidaftari cha kumbukumbu (autograph). Akamueleza anatamani kuwa dereva mkubwa wa magari ya McLaren na Dennis akamjibu Hamilton asijali watawasiliana ndani ya miaka 9 ijayo. Hiyo ikawa mwanzo wa safari ya Hamilton ya kuwa gwiji wa mbio za magari.

Baada ya kushinda mataji kadhaa akiwa kijana mdogo ikiwemo ya Super Series na la British Championship kwa mara ya pili mwaka 1998, McLaren akampigia Hamilton na kumsaini katika program za madereva watoto wa McLaren.

Ron

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Ron Dennis (kulia) bosi wa magari ya McLaren akiwa na Hamilton

Baada ya kupitia hatua kadhaa za mashindano, viwango na ujuzi ndani ya McLaren, na ukiacha ubinga Ulaya alioupata mwaka 2000 Hamilton alianza safari yake ya kushiriki mashindano makubwa ya Formula 1 mwaka 2007 akishinda GP2 Series.

Mwaka huo wa 2007, ndio mwaka uliomtambulisha rasmi kwenye ulimwengu wa mashindano makubwa ya dunia ya mbio za magari ya Formula 1, akiwa na dereva mwenzie Fernando Alonso.

Ulikuwa mwaka wa mafanikio na kushinda mara kadhaa kiasi cha kupewa mkataba mnono na McLaren wa miaka mitano ulioitwa ‘multimillion-dollar deal’ ambao ulikuwa unakoma mwaka 2012.

Baada ya mkataba wake kumalizika Hamilton alisainiwa na Mercedes akiendesha na pamoja na mkali mwingine Nico Rosberg, ambaye alikuwa rafiki yake wa tangu utotoni akaendelea kushinda kila mashanidano.

Mafaniko yake na utajiri

s

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lewis Hamilton akiwa na moja ya makombe aliyotwaa

Ushindi wa Lewis Hamilton katika mashindano ya Bahrain Grand Prix yanamfanya kushinda mbio mara 96 katika maisha yake ya mchezo huo.

Bingwa huyo mara saba wa dunia wa mbio za magari amekuwa akiweka rekodi mbalimbali za kuvutia.

Akishiriki Formula 1 kwa msimu wa 15, anakuwa muingereza wa kwanza kushinda angalau mara moja katika misimu yote. Rekodi inayomtofautisha na gwiji wenzake Michael Schumacher ambaye katika misimu 19 ameshinda katika misimu 15 mfululizo.

Mkataba aliousaini mwaka 2018 na Mercedes unamuingizia nyota huyo $55 million kila mwaka. Na katika maisha yake ya mchezo huo, amejiingizia kiasi cha $489 million.

Hamilton anatajwa kuwa mwanamichezo anaiyeshika nafasi ya 13 kwa wanaolipwa pesa nyingi Zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes akiingiza Zaidi ya $55 million kwa mwaka.

Ukiacha Mercedes kama dereva amekuwa na udhamini mnono akitangaza nembo za Mercedes-Benz, Tommy Hilfiger, Bose, Monster Energy, Sony, Puma na zingine zinazomuingizia mamilioni ya dola.

Hamilton ni mwanamuziki ‘nguli’ usiyemjua?

G

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lewis Hamilton (kulia) akiwa jukwaani na msanii Swizz Beatz katika moja ya matamasha ya Swizz

Pamoja na umaarufu wake na umahiri wake kwenye mbio za magari, Hamilton ana kipaji kingine ambacho sio wengi wanaokifahamu. Kipaji cha muziki. Unaweza kusema ni mwanamuziki alifichwa na umahiri wake kwenye magari.

‘Muziki ni kitu muhimu sana katika maisha yangu.”, Anasema Hamilton

Unaweza kuwa umesikiliza nyimbo za wasanii wakubwa kama Kanye West na Pharrell Williams na kukufanya ukaburudika, lakini Hamilton mkali asiyeficha mapenzi yake, akiiambia CBS kwamba hobi yake hiyo sasa ni kitu kinaanza kuwa “serious”.

f

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mwaka jana wakati anatambulisha nyimbo zake 8 alisema kwa miaka 10 amekuwa akiandika na kurekodi nyimbo lakini sio kwa ajili ya albamu.

Aliandika kwenye mtandao wake ‘Nimetumia miaka 10 zaidi kuandika na kurekodi, nikifanya kazi na wasanii wakubwa wenye vipaji, jambo ninalojivunia, alisema na kuongeza.Sina albamu, lakini nina nyimbo tu kadhaa ambazo unaweza kukugusa, zimenisaidia mie pia nilipopitia kipindi vigumu’

Hamilton alifichua pia kwamba yeye ndiye rapa XDNA aliyeshirikishwa kwenye wimbo uliotoka mwaka 2018 unaoitwa Pipe wa mwanamuziki Christina Aguilera.

Wengi hawakufahamu na hawakumfahamu XDNA, kumbe aliamua kuweka jina la bandia asijulikane, ingawa wachache waliomfahamu waligundua sauti yake.

Aliwahi kueleza pia alijenga studio kubwa ya muziki nyumbani kwaek kwa ajili ya mpenzi wake wa wakati huo aambaye wameshaachana Nicole Scherzinger, lakini mwishowe akaamua kuitumia mwenyewe na kupika nyimbo zake ambazo nyingi ni za mapenzi.

“Nilitengeneza studio kwa ajili ya Nicole, ili asiondoke kwenda Marekani kurekodi.” Lewis na Nicole walianza mahusiano mwaka 2007, kabla ya kutengana mwaka 2015.

Mvuto, Mahusiano yake na watoto

g

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mbali na magari, Hamilton ni mwanamitindo wa hisia, akipenda mitindo na kujiependa. Kwa umaarufu wake na kuvutia, haishangazi kuona wanawake wengi wakitamani kuwa nae kwenye mahusiano.

Nicole

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lewis na Nicole

Ukiacha mwanamuzi Nicole kutoka kundi la the Pussycat Doll, kwa mujibu wa mtandao wa essentiallysports, Hamilton amekuwa katika mahusiano na warembo kadhaa akiwemo Danielle Lloyd aliyedumu naye kwa miezi 6 mwaka 2002, na Jodia Ma aliyekuwa nae kwa miaka 4 mpaka 2007.

Nik

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Lewis na Mwanamuziki Nick Minaj

Aliwahi kutoka pia na mlimbwende Lotta Hintsa (Miss Finland), ambaye ni mtoto wa aliyekuwa msimamizi wake Aki Hintsa aliyefariki mwaka 2016, huku akitajwa kuwa na mahusiano na mastaa wengine kama Nicki Minaj, Rihanna, Vivian Burkhardt Rita Ora, Kendall Jenner, Barbara Palvin, Winnie Harlow na Sofia Richie.

Hakuna ripoti zinazomuonyesha kuwa na mtoto mbali ya kuoa, ingawa mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema amekuwa na mahusiano yenye matatizo yanayomfanya kuchelewa kupata mtoto.

“Ni vigumu kulinda uhusiano wako wakati unasafiri sana kama mie,” alisema na kuongeza “natamani kupata watoto, lakini nataka nisiwe ‘bize’ niwepo kwa ajili yao.”

CHANZO CHA HABARI BBC