Monday, October 18

Mchomanne United mabingwa bonanza la Bahari Fm Radio

MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, akimkabidhi shilingi laki saba (700,000) kepteni wa timu ya Machomanne United Seif Ali Hamad, baada ya timu yake kuibuka bingwa wa bonanza la Bahari FM Raido, kwa kuifunga Jamhuri bao 1-0 mchezo uliopigwa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja akisalimiana na mchezaji wa timu ya Machomanne United Abdul-mahfoudh Mohammed Ali kabla ya kuanza kwa bonanza la Bahari FM Radio, ambapo machomanne iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri mchezo uliopigwa Gombani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

NA ABDI SULEIMAN.

TIMU ya Mchomanne United imefanikiwa kutwa ubingwa wa bonanza la Bahari Fm Radio na kujinyakuliwa shilingi laki saba taslimi (700,000/=), baada ya kuichapa timu ya Jamhuri kutoka Wete bao 1-0 mchezo uliopigwa uwanja wa michezo Gombani.

Bonanza hilo lililokuwa na kauli mbiu yake “Nasimama na Rais Miwnyi kupinga vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar”liliweza kuvuta hisia za wapenzi wa soka na wadau wa bahari FM Radio Kisiwani Pemba.

Mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi wa soka, huku Mchaommne ikiwa katika maandalizi ya Ligi Kuu ya Zanzibar na Jamhuri ligi Draja la kwanza pemba.

Alikuwa ni mchezaji Hamad Said Othaman aliyeweza kupeleka fura kwa Machomanne United, baada ya kuipatia bao pekee timu yake na kupeleka huzuni katika mji wa Wete.

Mshindi wapili katika bonanza hilo timu ya Jamhuri iliweza kujinyakulia shilingi laki nne (400,000/=), huku Mchaomanne ikifanikiwa kuingia moja kwa moja katika bonanza kubwa la Bahari FM linatakalofanyika 2022.

Kwa upande wa ulaji wa maandazi kijana Hamad Khamis aliibuka mshindi wa kwanza kula maandazi matano, huku ufukuzaji wa kuku uwanawake akiibua Fatma Khamis Hamad, kwa upande wa uvutaji wa kamba kikundi cha Gombani kimeibuka bingwa katika mchezo huo.

Akifungua mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, aliipongeza Bahari FM Raido kwa kuandaa bonanza hilo, huku akiwataka kuendelea na kampeni zao ili kutokomeza matendo hayo ya udhalilishaji Zanzibar.