Tuesday, November 30

Miji juu ya maji…Je huu ndio mtindo ujao? Ni kwanini majaribio haya yajaribu mtindo huu katika nchi za Ulaya?

Mji

CHANZO CHA PICHA,OCEANIX / BIG-BJARKE INGELS GROUP

Kila mtu anafikiria kuwa suluhu bora ni kujenga majengo yanayoelea majini katika sikuzijazo ili kuweza kukabiliana na kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari na hali mbaya ya hewa inayoendelea kusababisha maafa duniani.

Unapowasili katika makazi yanayoelea ya Amsterdam nchini Uholanzi , utashangaa kuona watu wanaoishi katika jengo la gorofa linaloelea majini, wakifurajia hali ya hewa.

Unapowasili katika makazi yanayoelea majini ya Amsterdam utawaona wakazi hapa wameketi na kubembea kwenye benchi, wengine wakiendesha baiskeli na mtaa wa hoteli zinazouza nyama.

Kampuni ya Tan van Neymen , Montefloor, ilitengeneza mradi huu wa makazi ya ndani ya maji.

Mji wa Amsterdam

CHANZO CHA PICHA,ASHLEY COOPER / GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Mji wa Amsterdam

Tan van Nemen, ambaye alifanikiwa kujenga nyumba 100 zinazoelea ndani ya maji , anasema sio rahisi kubuni mradi wa majengo haya, lakini anasema ugumu wake haulingani na mafanikio yaliyofifgikiwa ya ujenzi huo.

Matatizo hayo ambayo yalisababisha kero kubwa sasa ndio sababu ya burudani, katika nchi hii ndogo ya Ulaya.

Hiyo ndio maanda Uholanzi sio tu nchi ya majaribio ya ujenzi wa majengo yanayoelea majini , bali Uholanzini sehemu ya majengo haya.

“Kulikuwa na tatizo la eneo wakati wa ujesnzi wa mradi huu ,” anasema Van Namen. Halafu mtu fulani akasema hizo nyumba zote ndani zinapaswa kuwa na urefu unaovuka viwango vya mtaa”. Alicheka kwa kicheko kikubwa Ivemo

Inafahamika kuwa Uholanzi pia inafanyia bahati yake ya ujenzi wa nyumba zinazoelea. Majaribio matatu yametokana na historia ya nchi yao ya ubunifu wa majengo.

Kupanda kwa viwango vya maji ya bahari vinaitishia Uholanzi.

Visiwa vya Reed vya watu wa jamii ya Uru kwenye ziwa Titicaca viko kwenye mpaka baina ya Bolivia na Peru

CHANZO CHA PICHA,SAIKO3P / GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Visiwa vya Reed vya watu wa jamii ya Uru kwenye ziwa Titicaca viko kwenye mpaka baina ya Bolivia na Peru

Mike van Wingarden, anaishi kilomita 55 kusini mwa Amsterdam, na hupitisha mifugo yake juu ya daraja na kuwapeleka katika zizi la kipekee linaloelea . Daraja hutumiwa kuwashushia ng’ombe kutoka kwenye meli za mizigo zinazotia nanga ndani ya maji

”Usiku mmoja kabla ya ngombe kuwasili, hatukuweza kulala . Lakini mchakato ulikwenda vyema , “alisema.

Uharibifu uliosababishwa na kimbunga cha mchanga katika mwaka 2012 lilivuruga kwa kiasi kikubwamfumo wa usafiri na usambazaji wa chakula katika New York.

Kwa siku chache zilizofuatia, maduka yote makubwa ya bidhaa katika Manhattan zilikuwa hazina bidhaa. Van Wingarden na mke wake walipata wazo la kutengeneza ”shamba linaloelea majini’.

Alipokuwa akirejea Uholanzi, aliamua kubuni shamba linaloelea majini rafiki wa mazingira.

Zizi la mifugo inayoelea

CHANZO CHA PICHA,JACK PALFREY

Maelezo ya picha,Zizi la mifugo linaloelea

Shamba hilo lililozinduliwa mwaka 2019, zizi linaloelea majini la ng’ombe lilitengenezwa . Wanyama hawa wanazunguka kwenye zizi hilo na maeneo mengine yanayoelea.

Shamba la kwanza la aina hiyo duniani kuwahi kubuniwa duniani. Shamba hilo huzalisha maziwa, jibini na yogati. Bidhaa hizi huuzwa kwa wateja wanaoishi katika maeneo ya karibu kwa baiskeli na mabasi madogo ya umeme.

“Shamba letu ni zuri kwa uzalishaji na tunauza vyakula vya afya.

Nadhani kutakuwa na mtizamo mzuri kwa aina hizi za mashamba yanayoelea siku zijazo , “alisema Van Wingarden. Anapanga kujenga shamba linaloelea la mboga pamoja na vibanda vya kuku.

Kutokana na mafanikio ya ”watu kuishi juu ya maji, uendeshwaji wa zizi la ng’ombe juu ya maji katika Uholanzi, maswali yanaibuka kuhusu iwapo miji yote itakuwa sawa na huu siku zijazo.

OCEANIX

CHANZO CHA PICHA,OCEANIX

OCEANIX

CHANZO CHA PICHA,OCEANIX

Kwa usaidizi wa Umoja wa Mtaifa , Shirika lenye makao yake makuu nchini Marekani, linaoitwa Oceanics linafanya juhudi na mipango ya kubuni makazi mengi na makubwa zaidi, imara na ya kisasa ya kijamii yanayoelea ndani ya maji yakiwa na nyumba 10,000 kwenye eneo la heka 75.

” Huku viwango vya maji ya bahari vikiongezeka, wale wanaoishi kwenye maeneo ya mwambao wana fursa ya pili. Makazi hayo ni jengo moja lenye ukuta mkubwa ambayo. hayapotezi uzito kutokana na ujenzi wa kisasa wa usanifu majengo wa hali ya juu , “alisema Mark Collinschen, Mkurugeni mkuu wa kampuni ya Oceanics.

Licha ya kuwa “Jiji linaloelea”, Oceanics pia inapendekeza kujenga wilaya pana. Miji kama Jakarta na Shanghai, ambayo inakabiliwa na matatizo ya kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari, inatarajiwa kufuata mtindo wa ujenzi wa miji inayoelea,

Miji mipya iliyobuniwa itajengwa kwa muungo wa pembetatu na upana wa heka mbili. Mradi huo umeundwa kuwa na makazi ya watu 300 kwa jila mji na kujengwa kwa klabu za sharehe na shughuli za kilimo katika eneo lililosalia la mji.

“Tunajenga jengo la kudumu ambalo linaweza kuhimili hali mbaya. Hatutaki kutumia makaa yam awe au gesi. Tutajaribu kubuni eneo litakalotimiza vigezo bya protini kwa 100% , “anasema Chen.

Yote haya yanafurahisha kuyaona na kuyasikia. Lakini je tunaweza kuona miji hii inayoelea ikijengwa kwa uhalisia katika kipindi cha maisha yetu?.

” Ha. Inaonekana. Katika kipindi cha miaka michache tutaona miji kadhaa inayoelea majini. Ninaamini hili kabisa, ” alisema Chen.

OCEANIX

CHANZO CHA PICHA,OCEANIX

Miji hii inayoelea ndiyo inayotufanya sisi tujihisi kama vitu vinafanyika katika hadithi. Lakini ukweli ni kwamba watu wamekuwa wakiishi katika makazi yanayofanana na haya kwa karne nyingi. Wakifanya shuguli za kilimo.

“Tumeandaa orodha ya maeneo 64 ambako duniani ambako watu wamekuwa wakiishi katika makazi yanayolea majini. Ukweli ni kwamba kinyume na miji yetu ya sasa, mifumo hii imekuwa ya kudumu kila mara, “alisema Julia Watson, mhadhiri wa ubunifu wa majengo na mwandishi wa kitabu cha Lotech katika Chuo kikuu cha Harvard.

Tunaweza bado kuona mifano ya jamii hizi zinazoelea. Visiwa vya Reed ni mfano wa mjamii zinazoelea katika Ziwa Titicaca kilichopo kwenye mpaka wa Bolivia na Peru

Bustani zinazoelea ni jambo la kawaida. Hizi zinaweza kuonekana hususan wakati wa vipindi vya upepo mkali katika Bangladesh.

Bustani inayoelea katika Bangladesh

CHANZO CHA PICHA,BENGAL PIX / ALAMY

Maelezo ya picha,Bustani inayoelea katika Bangladesh

Bustani inayoelea katika Bangladesh

” Inawezekana. Miji mingi duniani ina bandari. Pale unaweza kujenga miji sawa inayofanana. Kila mmoja duniani anataka aina hii ya majengo. Tatizo tunalokabiliana nalo sasa ni kuongezeka kwa viwango vya maji ambalo linaweza kutatuliwa kwa ujenzi wa miji kama hii inayoele”, alisema Julia Watson.