Monday, January 17

Maikel Osorbo: Rapa aliyeshinda tuzo ya Grammy akiwa gerezani nchini Cuba

Maelezo ya picha,Picha ya kwanza ya Castillo, ilichukuliwa kutoka kwenye sehemu ya video iliyochukuliwa mjini Havana.

Rapa raia wa Cuba Maykel Castillo, el Osorbo, hakuweza kuhudhuria tamasha za tuzo za Latin Gammy gala, Alhamisi huko Las Vegas ambapo wimbo ambao ameshiriki wa “Patria y vida”, ambao unaikosoa serikali ya Cuba na umepata umaarufu mkubwa, ulishinda tuzo mbili: Tuzo ya Wimbo Bora wa Mjini na Wimbo Bora wa Mwaka.

Kukosekana kwake Castillo kwenye tamasha hilo hakukutokana na Marekani kumnyima visa ya kuingia nchini humo, kama jinsi inavyotokea kwa raia wengine wa Cuba ambao wamekuwa wakiteuliwa kwa tuzo nyingine za matamasha zilizopita.

Rapa huyo muasi hakuweza kuhudhuria kwa sababu alifungwa tangu mwezi Mei kwenye gereza lenye ulinzi mkali nchini Cuba, akilaumiwa kwa kuhatarisha usalama wa umma na kuvuruga amani, baada ya kushiriki maandamano kadhaa kuipinga serikali.

Vyombo vya habari katika kisiwa hicho vinaeleza kuwa yeye ni mamluki na anawafanyia kazi CIA na maadui wa mapinduzi ambao kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, walihusika katika ushindi wa wimbo wa “Patria y life “will win in”

Ukweli ni kwamba Cuba ilishinda kwa mara ya kwanza katika historia ya tamasha hilo kwa wimbo wa mwaka na kwamba hili liliibua pingamizi kutoka kwa mamlaka ( katika kile ambacho kingekuwa ni sherehe kwa nchi nyingine)

Na ni kwamba Castillo, ambaye ndiye mwanamuziki wa kwanza katika historia ya tamasha hilo, kushinda tuzo mbili na kutoweza kupokea tuzo hizo kwa sababu ya kufungwa jela na katika hali mbaya ya kiafya, kwa mujibu wa mwanamuziki huyo mwenyewe na famialia yake na marafiki wa karibu.

“Anashinda tuzo wakati sio tu yuko gerezani na katika gereza leye ulinzi mkali, bali pia ni wakati ambapo hatma ya uchunguzi wa kesi yake haijulikani ni lini itafanyika lakini wakati pia yeye ni mgonjwa sana”, anasema Anamelys Ramos , mwanachama wa vuguvugu la upinzani San Isidro (MSI), ambalo pia Castillo ni mwanachama.

Kulingana na Ramos, Castillo ambaye anadai kuanza mgomo wa kususia chakula gerezani, kwa sasa anakataa kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu kwa sababu anaona kuwa kwa kuzuiliwa, hawezi kupata matibabu anayoyahitaji . Lakini mamlaka nchini Cuba hazizungumzii malalamiko kuhusu hali ya kiafya ya mwanamuziki huyo.

osorbo

CHANZO CHA PICHA,FACEBOOK/ANAMELYS RAMOS

Maelezo ya picha,Osorbo yuko gerezani katika jimbo la Pinar del Río, magharibi mwa Cuba.

Maykel “Osorbo” Castillo ni nani?

Alizaliwa Havana mwaka 1983. Hakuibuka tu kuwa kigezo cha muziki wa kuasi katika kisiwa hicho lakini pia mmoja wa wakosoaji wakubwa zaidi wa serikali.

Kulingana na vile aliiambia BBC miezi michache iliyopita, alikua bila wazazi katika kitongoji duni kwenye mji mkuu, alisoma hadi darasa la nne na kupitia vituo vya kuwarekebisha watoto mfano wa magereza ya watoto ambavyo vipo nchini Cuba na alipofika ujana ndipo alianza muziki.

“Alianza kuimba akiwa na umri mdogo na ndicho kitu anasema kilimuokoa kawa sababu alikuwa amefungwa kwa kupigana na vitu vingine kama hivyo. Aligundua kuwa alikua na kipawa na kwamba alikuwa na wajibu ndiposa akaanza kujulikana” anasema Ramos.

osorbo

CHANZO CHA PICHA,FACEBOOK/MAYKEL OSORBO

Maelezo ya picha,Osorbo alitoroka kutoka polisi na ke wake upande mwingine mwezi Aprioli mwaka jana

Anasema huo ndio wakati aliandaa tamasha kupinga kile kinaitwa Decree 349 iliyoidhinishwa na serikali kudhibiti malalamiko ya wasanii, na baadaye akaishia gerezani kwa mwaka mmoja unusu.

“Huo ndio wakati alifungwa jela kwa mara ya kwaza kwa sabbu za kisiasa, na ni wakati, baada ya kuondoka jela alishiriki zaidi katika vita vya kupigania haki za binadamu na kuhusika zaidi kwenye MSI, kwa mujibu wa Ramos.

Mwaka 2020 kundi lililowajumuisha wasanii wachanga wa upinzani na wasomi, walifanya mgomo wa kususia chakula ambao ulivunjwa na polisi na ambao ulisababisha maandamano mbele ya majengo ya wizara ya utamaduni mjini Havana.

Wakati alikuwa anakamatwa mwezi Aprili, Castillo aliokolewa na majirani walioandamana naye katika mtaa wa San Isidro.

Maisha

Mwanzoni mwa mwaka, alishiriki pamoja na rapa El Funki na kiongozi wa MSI, Luis Manuel Otero Alcantara, aliye pia gerezani, katika sehemu iliyorekodiwa nchini Cuba ya video “Patria y vida”, ambapo pia wanamuzki Yotuel Romero , Descemer Bueno na Gente de Zona walishirikia

Wimbo huo uliorekodiwa Havana na Miami unazungumzia baadhi ya matatizo yanayokumba kisiwa hicho yakiwemo hali duni ya makazi, uhaba wa chakula hadi mabadiliko ya kisiasa.

Wimbo huo ulipata umaarufu wa haraka na kutazamwa na mamiloni ya watu kwenye mtandao wa Youtube na kuwa kauli mbiu kwa wale walijitokeza kuandamana nchini Cuba wakati wa maandamano makubwa ya kuipinga serikali Julai 11.

Mamalaka nchini Cuba zinasema kuwa Osorbo sio mwanamuziki na kwamba yeye ni mamluki anayepokea pesa kutoka Marekani, anayefuata kanuni za CIA .

Ni kipi tena serikali inasema.

Mamlaka za kisiwa hicho zimeuelezea wimbo wa “Patria y vida” kama tambara na kuwaita waandishi wake panya, mamluki na maadui wa Cuba.

Gazeti la serikali lilihojia kuhusu tamasha hilo la kilatini la siku ya Ijumaa na kusema kuwa wimbo huo ulishinda kwa ujumbe wake wa kisiasa na wala sio kwa madili yake ya muziki.

Utata unaozunguka wimbo huo, ambao hauwezi kuchezwa kenye radio na televisheni za Cuba umafikia viwango vya juu zaidi nchini humo.

Díaz-Canel

CHANZO CHA PICHA,GETTY

Maelezo ya picha,Díaz-Canel aliteuliwa kuchukua nafasi ya Raúl Castro, ambaye alichukua mamlaka baada ya kuugua kwa kaka yake Fidel

Rais wa Cuba mwenyewe, Migeul Diaz-Canel ameukosoa kwenye mtandao wa twitter mara kadhaa na hata ameuzungumzia na viongozi wengine katika eneo hilo.

Kwenye mkutano wa Celac ulioandaliwa nchini Mexico, rais huyo alimshambulia hadharani rais wa Uruguay Luis Lacalle ambaye awali alikuwa amekariri mistari michache ya wimbo wa “Patria y vida.”

“Yaonekana kuwa Rais Lacalle ana kadha mbaya ya muziki, Wimbo huo ni uongo mtupu unaoendeshwa na baadhi ya wanamuziki dhidi ya mapinduzi ya Cuba,” alisema.

CHANZO CHA HABARI BBC/SWWAHILI