Monday, January 17

Matukio katika picha.

KUFUATIA jua kuwa kali na kiangazi kuwa kikubwa kupelekea majani au malisho ya wanyama kukauka, pichani Ng’ombe wakila takataka za mitaani pamoja na mifuko, kama wanavyoonekana katika picha huko Kijiji cha Uwandani Wilaya ya Chake Chake
MWANASHERIA kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Tawi la Pemba Safia Saleh Sultani, akitoa ufafanuzi wa maswali mbali mbali yaliyoulizwa na wananchi wa Uwandani, katika mkutano wa wazi uliondaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, ikiwa ni siku 16 za kupinga udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto
BAADHI ya wananchi wa Uwandani Wilaya ya Chake Chake, wakifuatilia mkutano wa wazi ulioandaliwa na Idara ya Katiba na msaada wa Sheria Zanzibar, juu ya siku 16 za kupiga udhalilishaji wa kijinsia
MENEJA wa Benk ya NMB Tawi la Pemba Hamad Mussa Msafiri (kushoto), akiwakabidhi shilingi Milioni tatu(3,000,000/=) wanakikundi cha Umoja ni Nguvu cha Mvumoni Chake Chake, ikiwa ni Bima ya mkono wa Pole kwa vikundi, inayotolewa na benk ya NBM baada ya mmoja ya wanakikundi hicho kufariki dunia
PO haja kwa wasimamizi wa sheria za barabarani kuwa makini wakati waote wanapokuwa katika majukumu yao, pia wananchi kufuata sheria za barabarani ili kunusuru ajali zisizokua za lazima, pichani wananchi/abiria wakininginia daladala yenye ruti Chake Chake-Wete licha ya kuwa imejaa jambo ambalo linaweza kusababisha ajali
AFISA Habari wa shirika la Umeme zanzibar Tawi la Pemba Amour Salum Massoud, akizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao na masheha wa Wilaya ya Chake Chake

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)