Monday, January 17

Rais Dk Hussein Mwinyi ahudhuria taarab rasmi ya kikundi cha taifa kusheherekea Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni kuhudhuria hafla ya Taarab rasmin ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika jana usiku,12-1-2022.(Picha na Ikulu)

/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amisimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar na Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar, kabla ya kuaza kwa Taarab rasmin  ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WASANII wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar wakipiga wimbo wa Taifa wa Zanzibar kabla ya kuaza kwa Taarab rasmin ya Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika jana usiku,12-1-2022 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi.Fatma Hamad Rajab, akisoma ratiba ya Taarab Maalum ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MSANII Nassor Hussein akiimba wimbo wa Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa hafla ya Taarab Rasmin ya kusherehekea  maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar wakitowa burudani, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

/MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akijumuika na Wananchi katika Taarab Maalum ya Kikundi cha Taifa cha Zanzibar na (kulia) Mhe Asha Abdalla Juma , katika taarab rasmin ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usiku 12-1-2022.(Picha na Ikulu)

MSANII Profesa Mohammed Elias akitoa burudani wakati wa Taarab rasmin ya Kikundi cha Taifa cha Zanzibar akiimba wimbo wa Nimesafi Moyo , wakati wa hafla ya Taarab ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar , iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usiku 12-1-2022.(Picha na Ikulu)

NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma na (kushoto) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakifuatilia hafla ya Taarab Rasmin ya Kikundi cha Taifa cha Zanzibar,  kusherehekea maadhimisho ya Miaka  58 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usiku 12-1-2022.(Picha na Ikulu)

MSANII wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar Amina Abdalla akiimba wimbo wa Kibali wakati wa Taarab rasmin ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MSANII wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar Amina Abdalla akiimba wimbo wa Kibali wakati wa Taarab rasmin ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitabasamu na kufurahia jambo wakati wa hafla ya Taarab Rasmin ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar wakitowa burudani katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na (kulia) Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita.(Picha na Ikulu)

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akifuatila hafla ya Taarab Rasmin ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar  na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia, ilioandaliwa maalum kwa ajili ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil, Kikwajuni jijini Zanzibar, ambapo magwiji wa sanaa ya muziki wa  Taarabu asilia kutoka Kikundi cha Taifa Zanzibar, walionyesha umahiri wao katika kuchararaza nyuzi na kughani nyimbo mbali mbali na kukonga nyoyo za mashabiki wa sanaa hiyo kutoka Mikoa yote ya Zanzibar.

 

Katika burudani hiyo nyimbo mbali mbali zilizopata kuvuma na kupendwa kutoka kwa watunzi wabobezi na waimbaji nguli wa sana hiyo zilipata fursa  ya kuimbwa na kuibua vifijo na nderemo.

 

Nyimbo ya kwanza ambayo ilifungua pazia la burudani hiyo, ilikuwa ni ile ilioendana na maudhui ya sherehe hizo, ambapo Mwimbaji nguli Al-anisa Fatma Dawa alighani kwa ustadi mkubwa na kuwafanya watazamaji kuinuka kwenye viti na kumtunza.

 

Aidha, kumalizika kwa nyimbo hiyo, kulitoa fursa kwa mwimbaji mahiri Al – anisa Hilda Mohamed kughani nyimbo maarufu na iliowahi kupata sifa kubwa hapa Zanzibar, ijuilikanayo kwa jina la ‘Nisubiri hadi lini’.

 

Kadri muda ulivyosonga, ndivyo Burudani hiyo ya taarabu  iliendelea kunoga  na kuufanya usiku huo kuwa maalum kwa wapenzi na mashabiki wa sanaa hiyo, hususan pale zilipoimbwa nyimbo maarufu kama vile, Cheo chako, Kibali, Kweli ninae, Mpewa hapokonyeki, Lulu, Ubinafsi na choyo, Lipi nilopenda kwako na kuhitimishwa na nyimbo ya Wahoi.

 

Nyimbo nyengine zenye mnasaba na maudhui ya  sherehe hizo ambazo zilipata nafasi ya kuimbwa na kuibua  shwangwe kubwa, ni pamoja na ile ya kumpongerza Dk. Mwinyi kwa Uongozi wake, ilioimbwa na msanii nguli  Nassor Hussein.

 

Katika hafla hiyo, ambapo Rais Dk. Mwinyi aliambatana na Mama Mariam Mwinyi,  watazamaji na mashabiki wa sanaa ya taarabu asilia walikoshwa na kupata kile mioyo yao inapenda, baada ya kuwashuhudia wasanii nguli kama vile Ustadh Idd Sued (mpendwa na wengi) na Profesa Mohamed Elias wakiendelea kuimba kwa sauti ile ile iliyozoeleka kwa miaka na dahari na kuthibitisha ule usemi wa ‘vya kale ni dhahabu’.

 

Viongozi mbali mbali wa Kitaifa, akiwemo Makamo wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdalla walishiriki.

 

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar