Sunday, June 26

Wadau waishukuru idara ya msaada wa kisheria

 

 

NA ABDI SULEIMAN.

KUZINDULIWA kwa Muongozo wa uanzishwaji wa vituo vya msaada wa kisheria katika vyuo va vituo vinavyotoa mafunzo ya kisheria na Muongozo wa upatikanaji wa msaada wa kisheria Vizuizini, itaweza kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi za kuhudumia wananchi.

Walisema kuwepo kwa miongozo hiyo ni jambo la faraja kwao, walioko vizuwizini wataweza kupata haki zao za kisheria pale wanapoona haziendi sawa.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, mjini Chake Chake wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo hiyo, wamesema sasa mabadiliko makubwa yatatokea katika kazi zao.

Msaidizi wa Sheria Jimbo la Ziwani Hadija Said Khalfan, kuzinduliwa kwa miongozo hiyo itaweza kuwasaidia wananchi wenye vizuizi kupata haki zao, jambao ambalo hapo kabla walikuwa wakilikosa.

“Kabla watu walikuwa hawapati haki zao, sasa haki zao zinapatikana ikiwemo ukataji wa rufaa na masuala mengine yanayohitaji masuala ya kisheria”alisema.

Naye Mratibu wa baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Mashavu Juma Mbarouk, aliishukuru idara ya katiba na msaada wa Kisheria Zanzibar, kuanzisha miongozo hiyo itayoweza kuwasaidia watu wenye umelavu kupata haki zao za kisheria.

Alisema watu wenye ulemavu wakilikuwa wakikosa haki zao mbali mbali za kisheria, na kupelekea kudhulumiwa mambo mbali mbali wanayoyahitaji.

Akiwasilisha muongozo wa upatikanaji wa msaada wa kisheria vyuo vikuu na vituo vinavyotoa mafunzo ya sheria, Salma Suleiman Abdullah kutoa idara ya Katiba na Msaada wa kisheria.

Alisema upatikanaji wa msaada wa kisheria unalenga kuwafikia, wananchi wanaishi katika maeneo ya mjini na Vijijini kwa kutoa haki sawa.

Akizungumzia malengo ya uanzishwaji wa vituo vya utoaji huduma za msaada wa kisheria, alisema kutoa na kusaidia upatikani wa huduma za msaada wa kisheria kwa watu wasiokua na uwezo na wenye mahitaji maalumu, kutoa elimu ya kisheria na uhamasishaji na kushirikiana na wasaidizi wa kisheria katika shehia zao.

Naye Moza Rajab Baraka kutoa idara ya katiba na msaada wa kisheria, wakati akiwasilisha muongozo wa upatikanaji wa msaada wa kisheria vizuizini, alisema uwepo wa muongozo huo utaweza kuwasaidia wananchi waliopo vizuwizini kupata haki zao za kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema wasaidizi wa sheria wanapaswa kufuata taratibu na kanuni za sehemu husika.

Alisema wasaidizi wanapswa kufika mapema sehemu ambayo wanahitaji kutoa huduma za kisheria, ili kuweza kujua taratibu zote za sehemu hiyo.

MWISHO