Friday, August 12

KAMISHNA Awadhi atoa muarubaini kwa mashahidi wanaokataa au kutoa ushahidi wa uongo kesi za udhalilishaji Pemba

NA KAILANI JUMA .

KAMISHNA wa Polisi Zanzibar Awadhi Juma Haji Amemuagiza kamanda wa polisi Mkoa wa kusini Pemba, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, Mashahidi ambao hawakutaka kutoa Mashirikiano ama kutoa ushahidi wa uongo katika kesi za udhalilishaji Mkoani humo.

Amesema Kuna kesi ambazo hazikuendelea mahakamani kutokana na mashindi kushindwa kwenda kutoa ushahid na wengine kutoa ushahid usio kuwa wakweli wanapo kuwa mahakamani tofauti na wanaporipoti kesi hizo Hivyo sasa kesi hizo zitafuatiliwa na Kila ambaea kafanya Hivyo atachukuliwa Sheria

Kamishina Awadhi ametoa magizo hayo Huko makao makuu ya polis mkoa wa kusini Pemba akizungumza na masheha na askari shehia wilaya ya chake chake.

amesema jeshi la polis halitasita  kuwachukulia hatua wale wote  wanao singiziana kesi za udhalilishaji kutokana na chuki zao binafsi kwakua  serekali zinazichukulia Kwa umakini kesi hizo.

Aidha amesema serekali imekuwa ikifanaya Jitihada za kumaliza kesi hizo ila suala la muhali limekuwa likirudisha nyuma suala Hilo Hivyo sasa inataka kuondoa muhali huo Kwa kutumia Sheria.

Pia amemtaka kamanda wa polis kuwachukulia hatua wanaochezesha michezo ya kamari (GEME) Kinyume na Sheria katika majumba Yao

Amesema katika kuimarisha uslama wa raia jeshi la polis  linajipanga kuimarisha vituo vidogo vidogo Vya polis ndani ya wilaya ya chake chake kutokana ukubwa wa eneo la wilaya hiyo.

Ameongezea kuwa masheha wanawajibu mkubwa wa kushirikiana na na jeshi la polis katika kupiga vita uhalifu wowte ndani ya shehia zao

Amesema Jeshi la polis halitasita kumchukulia hatua mtedaji wowote wa polis ambaye anaenda Kinyume na Sheria katika mapambano ya kupiga vita kesi hizo.

Kwa upande wake kamanda wa polis mkoa wa kusini Pemba Richard thedeo mchovu Amewataka askari shehia kutoa kipao mbele suala la kuwapa Elimu ya kudumiaha Amani na usalama wa raia na mali zao.

Nao masheha hayo wamemuomba kamishina huo kuwaongezea Askari shehia kutokana na askari mmoja kuwa na shehia Zaid ya mbili.

Kamishina Awadhi yupo mkoa wa kusini Pemba Kwa ziara ya siku mbili kuzungumza na wanajamii pamoja na viongozi mbali mbali wa serekali katika kuimarisha amani na usalama.

 

  MWISHO