Friday, September 29

WAFANYA USAFI KUELEKEA SIKU YA USHIRIKA.

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, amewataka wananchi wa wilaya wa kisiwa cha Pemba kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya makaazi ili kupunguza maradhi mbali mbali ikiwemo nyemelezi.

Mkuu huyo alisema iwapo wananchi watasafisha mazingira katika maeneo yao, wataweza kupunguza hasara kubwa ya maradhi nyemelezi katika maisha ya kawaida, kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Aidha mkuu huyo aliyaeleza hayo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi wa mazingira, katika barabara ya pangali pondeani, ili ni kuelekea siku ya ushirika duniani.

Alisema unapoboresha usafi unaboresha kinga katika maeneo yetu, pamoja na kupunguzia mzigo serikali kutibu, wakati fedha hizo ilizipanga kwa shuhuli nyengine na sio matibabu hayo.

“Elimu hii tulioipata leo tukaitekeleze kwa vitendo, kila mmoja kuchukua kwa jukumulake kufanya usafi katika ngazi ya familia, usafi ndio kila kitu kwa sasa,”alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kushikamana kudumisha usafi, kwani bila ya usafi hakuna utalii na watalii wanavutiwa na usafi wa maeneo husika.

Alisema watalii wanaangalia usafi wa mazingira, chakula na sehemu za malazi, hivyo ili kuwavutia watalii lazima mazingira yaendele kuwa safi muda wote.

Akizungumzia siku ya ushirika, Mkuu huyo aliwashukuru watu wa ushirika kwa kuwaunganisha, kwani ushiorika unanafasi yake katika kuhakikisha jamii inapata huduma, jamii inakua na kua na sauti ya pamoja katika kutetea mambo mbali mbali.

Wamefarajika sana kupata siku ya ushirika duniani kufanyika kisiwani Pemba, kila mmoja kufanyavizuri wataweza kupiga hatua katika masuala mbali mbali.

Kwa upande wake mkurugeni vyama vya ushirika Zanzibar Khamis Dadi Simba, alisema siku hiyo ni siku adhimu iliyotangazwa baraza la umaja wa matifa, wanaushirika kufanya masuala mbali mbali ya kijamii.

Alisema madhumuni makubwa ni matatu moja ni kupeana elimu, wanaushirika kukaa kutathimini juu ya vyama vyao kuona inavyonyanyua hadhi ya utu pamoja na maunganisho.

Aidha alisema usafi ni muhimu na kuepeana mafunzo kwa vitendo kwa kutengeneza kanuni, pamoja na maagizo ya Rais katika suala zima la usafi.

Naye Mkurugenzi wa Baraza la Mji Chake Chake Maulidi Mwalimu Ali, aliwashukuru wasanii kwa kushirikiana katika usafi wa eneo hilo, kwani kama wangefanya wao wamengefanya kwa mwezi mzima.

“Leo eneo la mita 200 tumefanya usafi hii sio sehemu ndogo, tumefanya kwa pamoja na tumeweza kusafisha kwa kufeka na kufagia hili ni jambo kubwa,”alisema.

Kwa upande wake katibu wa shirikisho la wasanii Pemba Salum Nassor Suleiman, alisema wapo tayari kushirikiana katika masuala mbali mbali ya serikali na jamii katika suala zima la usafi.

MWISHO