Tuesday, October 4

FCS migogoro haipaswi kupewa kipaombele njia mbala zinapaswa kutumika

 NA ABDI SULEIMAN.

TAASISI ya Foundation For Civil Society Tanzania, imesema migogoro inayotokea katika jamii haipaswi kupewa kipaombele kwani inapelekea uvunjifu wa amani, amani ambayo inapaswa kulindwa na watu wote na sio mtu mmoja pekee.

Hayo yameelezwa na afisa miradi kutoka FCS Eveline Mchau, wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Chake Chake, baada ya kumalizika kwa mafunzo juu ya mbinu za utatuzi wa migogoro kwa shehia tano zilizomo ndani ya wilaya hiyo na kuandaliwa na KUKHAWA.

Alisema migogoro inayoleta uvujifu wa amani sio ya kisiasa pekee yake, bali hata migogoro ya ardhi, udhalilishaji wa wanawake na watoto jambo ambalo hupelekea uvunjifu wa amani katika jamii.

“Viongozi wa shehia wasipokaa pamoja na wananchi wao, masuala yote ya mtambuka yanayotokea na wasipo yafanyia kazi basi, hawatendei haki wananchi wanaowahudumia,”alisema.

Aidha aliwataka viongozi hao kuyafanyia kazi mafunzo ya utatuzi wa migfogoro, ili kuwa salama na jamii yao kwani mradi wa dumisha amani, una namna nyingi na kufikia makundi mengi tafauti kwa ajili ya kufikia jamii.

“Masheha na viongozi wa dini, viongozi wa serikali, vijana na makundi mbali mbali, kwa ajili ya kuwapatia elimu juu ya utatuzi wa migogoro namna ambayo ni muhimu,”alifahamisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa KUKHAWA Hafidh Abdi said, aliishukuru FCS kwa kuzisaidia NGOs za zanzibar, huku akiwataka washiriki kwenda kuyafanyia kazi mafunzo waliopatiwa, ili jamii iliyokubwa iweze kunufaika.

Alisema matatizo yaliyoko katika shehia waanapaswa kutumia njia mbadala kutatua, mambo makubwa ambayo hawayawezi wanapaswa kuwasiliana na KUKHAWA, ili isije ikawa ndio chanzo cha migogoro kwenywe jamii.

Naye mwakilishi kutoka ofisi ya mrajis wa NGOs Pemba Sada Aboubakar Khamis, alisema KUKHAWA ni moja ya jumuiya bora zinazo saidia jamii, kwani kwenye jamii kuna migogoro mingi na inahitaji kutatuliwa na watatuani ni masheha wa shehia kabla kufikia kwenye vytombo vya sheria.

“Niwakati sasa kutumia njia shirikishi katika utatuzi wa migogoro, ili kuleta manuafaa, sisi tuliochagulia ni wachache tunakutana na jamii kubwa na tusiwe chanzo cha kuazisha au kuibua hiyo migogoro katika jamii,”alisema.

Akiwasilisha mada njia mbadala za kusuluhisha migogoro Mwanasheria Siti Habibu Moh’d, aliwataka washiriki hao kuhakikisha wanafuata njia mbadala za usuluhishi wa migogoro na sio kukimbilia kwenye vyombo vya sheria.

Alisema mahakama zinapendelea migogoro itatuliwe kwa njia mbadala kama vile usuluhishi ili kuepusha mrundikano wa kesi mahakamani, kwani hapo kila mmoja anaweza kupata haki yake tafauti na kukimbilia kwenye vyombo vya sheria.

Nao washiriki wa mafunzo hayo, walisema suala la mirathi limekua likichangia kwa akiasi kikubwa kutokea kwa migogoro ya ardhi katika jamii, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kudumisha amani na utulivu iliyopo nchini.

MWISHO