Tuesday, October 4

NMB yakabidhi madawati yenye thamani ya milioni 17 Kojani

 

NA ABDI SULEIMAN.

MKUU wa idara ya huduma za Serikali kutoka NMB makao makuu Vicky Bushubo, amesema NMB inatambua kazi nzuri na mchango mzuri unaofanywa na serikali ya SMT na SMZ, katika suala zima la kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya elimu na afya nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo, nayo NMB imekua msatri wambele kusaidia huduma mbali mbali za jamii, pale wanapoombwa kusaidia ikiwemo madawati 150 yenye thamani ya shilingi Milioni 17 waliokabidhi Kisiwani Pemba.

Mkuu huyo aliyaeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Pemba, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi madawati kwa skuli tatu zilizomo ndani ya jimbo la Kojani.

Alisema kwamba wanafanya hivyo kutokana na wanatambua, kuwa wanawajibu wa kurudishia faida wanayopata kwa jamii, kwani maendeleo ya bank yao yanachangiwa na kazi nzuri inayofanywa na wananchi popote walipo nchini Tanzania.

“Tumekua tukifanya kazi kwa karibu sana na wananchi na wadau wetu hapa Pemba, kwa kweli hali halisi iko vuzuri na tumejikita kusaidia sana jamii yetu,”alisema.

Alifahamisha kwamba Pemba mwitikio wa huduma za fedha ni mkubwa sana, wanawateja elfu 25000 na wameweka amana inayofikia Bilioni 15 katika bank hiyo.

Akizungumzia suala la mikopo, alisema wananchi wameitikia vizuri masuala ya kukopa, tayari wameshakopa shilingi milioni 10 na wanamawakala wapatao 25, huku wakiwa na mipango mizuri ya kufungua tawi Wete.

Kwa upande wake Meneja huduma za biashara NMB Zanzibar Naima Said Shaame, alisema NMB ipo karibu na jamaii na wanasaidia jamii, kwani wametenga asilimia moja ya faida wanayoipata wanairudisha kwa jamii.

Akizungumzia suala la maombi alisema wanajikita katika elimu na maombi yamekuja jimbo la kojani, huku akiwataka walimu wakuu kupeleka maombi katika matawi yao kwani mwaka 2022 wametenga bilioni 2 kusaidia jamii.

Naye meneja ya NMB Tawi la Pemba Hamad Msafiri, aliwataka wananchi kuyunga mkono benk hiyo, ili kuweza kupata mikopo na huduma nyengine mbali mbali ikiwemo bima.

Nao walimu wa skuli ya Kojani, chwale na jojojo, waliishukuru benk hiyo kwa juhudi zao za kusaidia huduma mbali mbali za kijamii, huku wakizitaka taasisi na mashirika mengine ya kibenk kujitokeza kusaidia huduma za elimu.

MWISHO