Tuesday, February 7

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 30.11.2022

Harry Kane

Bayern Munich wako katika harakati ya kumnunua mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 29, katika klabu hiyo kwa mkataba ambao unaweza kugharimu kati ya euro 80m na ​​100m. (Sky Sports Germany)

Tottenham wamefanya uchunguzi kwa Inter Milan kuhusu mlinzi wao wa pembeni wa kimataifa wa Uholanzi, Denzel Dumfries, 26. ((90 min)

Mustakbal wa baadaye wa mlinda lango wa Senegal Edouard Mendy, 30, na Mhispania Kepa Arrizabalaga, 28, katika klabu ya Chelsea uko shakani huku klabu hiyo ikifikiria kuleta mlinda mlango mpya ambaye atakuwa chaguo la kwanza msimu ujao wa joto. (Sun)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Cristiano Ronaldo

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn anasema klabu yake haitamsajili fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, mwezi Januari kufuatia kuondoka kwake Manchester United. (Sky Germany, via Mirror)

Kahn pia anasema klabu hiyo ya Bundesliga itaketi na fowadi wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting, 33, kujadili mkataba mpya baada ya Kombe la Dunia, kwani mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika msimu wa joto. (Fabrizio Romano)

Roma wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 25 katika msimu wa joto. (Calciomercato – In Italian )

.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,Lionel Messi

Mshambulizi wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, anatarajiwa kusalia katika soka la Ulaya angalau hadi 2024, licha ya ripoti kuwa anakaribia kukubali dili la kujiunga na klabu ya MLS Inter Miami mwaka ujao. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa zamani wa England Joe Cole anasema mshambuliaji wa Uholanzi na PSV Cody Gakpo, 23, atakuwa “kwenye rada za vilabu vyote vikubwa” baada ya jukumu lake la kulisaidia taifa lake kwenye Kombe la Dunia. (ITV, Via TalkSPORT)

Aliyekuwa mkufunzi wa Sheffield United Chris Wilder anavutiwa na kibarua kilichoachwa wazi cha Queens Park Rangers baada ya Michael Beale kuacha jukumu hilo kwa Rangers. (Sun)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie amekuwa funguo muhimu kwa Milan kuanza vyema Serie A, huku klabu hiyo ikimenyana na Roma siku ya Jumatatu.

Inter Milan wanafikiria kuwasilisha ombi la kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Ivory Coast Franck Kessie, 25, msimu ujao. (Calciomercato – In Italian)

West Ham wamemwambia kiungo wa kati wa Ireland Conor Coventry, 22, kwamba yuko huru kupata klabu mpya kabla ya dirisha la uhamisho la Januari. (Football Insider)

CHANZO CHA HABARI BBC NEWS SWAHILI.