Tuesday, February 7

Wanaharakati wanaopinga vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto waomba mifuno ya takwimu ionyeshe uwazi wa kesi.

NA ABDI SULEIMAN.

WANAHARAKATI wanaopinga Vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto Pemba, wameiyomba serikali na mamlaka husika kuimarisha mifumo yake ya takwimu za matukio hayo, ili zioneshe kwa uwazi mwenendo wa kesi hizo na idadi ya kesi zilizotolewa maamuzi katika kila kipindi, ili kutoa mwelekeo halisi wa matukio hayo.

Wakizungumza na waamdishi wa habari Kisiwani hapa, katika ofisi za TAMWA Pemba, wanaharakati hao wamesema mifumo hiyo ya takwimu za matukio hayo, zitasaidia kujamii kujua mwenendo mzima unavyoenda na kesi zilizotolewa maamuzi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Nassor Bilali Ali, alisema asasi mbali mbali za kiraia Pemba, zimeungana kwa pamoja kuhakikisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike unakomeshwa nchini.

Alisema katika kuelekea siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawak na watoto wa kike, wameshauri serikali mahakimu wanaofanya vizuri katika uzimamizi wa kesi pamoja na kuwachukulia hatua wale wanaochelewesha keshi hizo kwa makusudi.

“Watakapochukuliwa hatua wanaochelewesha kesi za ubakaji na udhalilishaji wa wanawake na watoto, kuwepo kwa mpango maalumu wa kuwatambua ili kuweka uwajibikaji wa pamoja katika uendeleshaji wa kesi hizi,”alisema.

hata hivyo alisema asasi za kiraia zina amini iwapo kutakuwa na mifumo imara, inayosimamia uwazi wa takwimu zenye kutoa mchanganuo wa mwenendo na idadi ya kesi, zilizochukuliwa hatua na zilizofutwa itachochea uwajibikaji katika kufanikisha juhudi za Rais wa Zanzibar Dkt.Husein Ali Mwinyi kuanzisha mahkama maalum ya kesi za udhalilishaji.

Hata hivyo aliyomba jamii kupunguza muhali na badala yake iwe msitari wa mbele, kuripoti matukio haya kwa wakati yanapotokea na kuwa tayari kutoa ushahidi wanaohitajika kwenye vyombo vya sheria, ili kufanikisha hatua kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa.

Katika hatua nyengine alisema kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa, imeonekana kuna umuhimu wa pekee wa kuwepo kwa kipindi maalum cha kutafakari na kufanya kampeni za makusudi za kupinga ukatili huo.

kwa mjibu wa ripoti ya takwimu za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar, kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali zanzibar kwa mwezi wa agositi 2022, jumla ya matukio 131 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi huo, waathirika Wanawake ni 12 sawa na 9.2% na watoto ni 119 sawa na asilimia 90.8, miongoni mwao wasichana walikuwa 84 (asilimia 70.6% na wavulana walikuwa 35 sawa na 29.4%.

 

Asasi za kiraia kisiwani zilizoungana ni Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, KUKHAWA, ZAPDD, blog ya Pemba Today, Jumuia za wasaidizi wa sheria za wilaya nne za Pemba, PEGAO, TUJIPE, ZYCO, MY HOPE FOUNDATION, PAFIC.

MWISHO