Sunday, March 26

ASASI ZA KIRAIA ZATAKIWA KUJIKITA ZAIDI KUELIMISHA ATHARI ZA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

 

Na shaib kifaya Pemba.

Afisa MdhaminiWizara ya afya Kisiwani Pemba Dr. khamis Bilali Ali, amewataka wanaharakati wa asasi za kiraia wa kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kuendelea kuelimisha Jamii katika kujikinga na kujiepusha na madhara ya matendo hayo.
Kauli hiyo ametoa hako ukumbi wa Samail Gomban Chake chake kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Abdalla Rashid Ali, katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga  ukatili na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na watoto.
Alisema chimbuko la maadhimisho hayo linatokana na tamko La katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan  la mwaka 2006 kwa mataifa yote kujua ukubwa wa tatizo la ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wakike.
Afisa Mdhamini huyo alisema vitendo vya udhalilishaji bado nitatizo kubwa na matukio haya yanaongezeka na kuripotiwa siku hadi siku katika Jamii
Alifahamisha matukio hayo yanashindwa kumalizika kutokana  na changamoto mbali mbali ikiwemo kwa baadhi ya Jamii kutotoa mashirikiano mazuri na vyombo vya sheria vinavyo simamia matukio hayo
Akisoma taarifa fupi ya kazi  za asasi za kiraia  kuanzia November 25- hadi disemba 10 mwaka huu Tatu Abdalla Mselem kutoka Tumaini Jipya Pemba ,alisema  wamefanya kazi kubwa ya kuelimisha umma kwa Wilaya zote 4 za Pemba kuelezea madhara ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia .
Aidha alifahamisha kwamba chimbuko la siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia linatokana na mauaji ya kinyama  ya wasichana Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominic mwaka 1960 walo dai haki zao .
Kwa upande wake afisa miradi kutoka SOS Pemba Abdalla Omar Kidim, alisema wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kushirikiana na asasi za kiraia kwa maeneo mbali mbali hasa katika kumlinda mtoto na matukio ya udhalilishaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Hata hivyo alisema siku 16 hutoa mwanga kwa Jamii kwani ni siku muhimu ambapo itakumbukwa disemba 6 ni siku ya mauaji ya kikatili ya wanawake 24 waliuliwa na MTU aliye wachukia wanawake duniani .
Nae Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Pemba Omar Mohammed Ali alizishukuru asasi za kiraia kwa kazi nzuri ya utoaji wa elimu kisiwani Pemba kwani wamekuwa wakisaidia Wizara ya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto
Taasisi ziloshiriki kuotoa elimu ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia katika siku 16 ni Tamwa,Tujipe, Kukhawa, Pagao, ZLS,ZYCO, Chapo na My Hope Foundation.
Mwisho.