Sunday, March 26

YANGA SC YAICHAPA IHEFU FC 1-0, YAKICHIMBIA KILELENI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga Sc imefanikiwa kulipa kisasi kwa kuichapa Ihefu Fc kwa bao 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam..

Katika mchezo huo, tumeshuhudia mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Kalala Mayele ameweza kuongeza kalama yake ya mabao baada ya kufunga kwenye mechi hiyo.

Mchezo wa kwanza mzunguko wa kwanza Yanga iliharibiwa Unbeaten ya 50 na kufikia 49 kwa kufungwa bao 1-0.