Sunday, March 26

YANGA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0, YAENDELEA KUSALIA KILELENI

NA EMMANUEL  MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya yanga imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi kuu tanzania bara baada ya kufanikiwa kuondoka na alama  tatu mbele ya Ruvu Shooting kwa kuichapa bao 1-0,  mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini  Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo  huo  Ruvu Shooting walijifunga kupitia  kwa beki wao wa pembeni Mpoki  Mwakinyuke  akijaribu kuokoa hatari mbele ya mshambuliaji wa yanga Kenneth Musonda na kutinga moja kwa moja wavuni.

Yanga Sc imeendelea  kuwakosa wachezaji wao kadhaa akiwemo Nkane, Aucho, Morrison na Mshery ambao wamekosekana kwa sababu tofauti tofauti.