NA THUREYA GHALIB- PEMBA. .
Kuna Msemo usemao Adhabu ya kaburi aijuaje maiti huu ni msemo unaofahamisha kuwa aliyefikwa na shida fulani ndiye anaejua na kufahamu shida ya jambo husika.
Au pia kuna msemo unaosema aisifuye mvua imemnyeshea,msemo huu unamana kuwa kila jambo ambalo mtu analizingumzia atakuwa aidha ana uzoefu nalo kwa namna moja au nyengine analifahamu.
Hii ni misemo inayonesha ni jisi gani Mtu anapopata matatizo unatakiwa umskilize na kumpa faraja maana yeye ndie mtu pekee anaehisi uchungu wa Jambo hilo.
Leo Katika Makala haya nimelenga kuzungumzia ni kwa namna Gani ukosekanaji wa Fidia kwa Wahanga wa Kesi za udhalilishaji unavosokota mioyo yao .
Nini maana ya malipo ya fidia?
Maana ya malipo ya fidia kikawaida fidia inarejelea malipo ya pesa yanayotolewa kwa mtu binafsi badala ya huduma zake Katika sehemu za kazi.
Fidia ni ile inayopatikana kwa wafanyakazi, inajumuisha mshahara pamoja na kamisheni na motisha au marupurupu yoyote yanayoambatana na nafasi ya mfanyakazi aliyepewa.
Au kwa maana nyengine fidia tunaweza kuielezea kuwa ni Malipo yanayotolewa kwa mtu aliesababishiwa maumivu au hasara ya kitu Fulani.
Je?Kwa upande wa Mahkama inajulikana Vipi Fidia?
Kwa Upande wake Kaimu Mwanasheria Dhamana kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Pemba Seif Mohamed Khamis alisema Fidia nikama nafuu au malipo yanayotolewa na Mshtakiwa kwa muathiriwa kama nafuu kwa kupunguza yale makali ya uhalifu anayoyapata ,kuna wengine wanathirika kiakili au kimwili.
Sikwamba hio nafuu(fidia) inayotolewa inakuja kuponyesha lile jeraha analolipata muhanga hapana lakini ni makisio ambayo yataweza kumsaidia yule muhanga .
Mara nyingi changamoto ya ulipaji fidia inakuja kuwa shida yule anaetakiwa kulipa wapi atatoa ile pesa ya kulipa, hio ni kutokana na hali ya kiuchumi kuwa duni.
“Mara nyingi mshtikiwa anakuwa hana njia ya kupata kipato, wanatoka katika Maisha ya kawaida ambayo hajajipangia mustakabali mzuri wa maisha yake”Alisema Seif
Hivyo Kama mtu anajulikana anakipato na ana uwezo wa kulipa fidia na inakuwa rahisi zaidi kukumbana na kumsimamia alipie fidia hio, katika nchi za wenzetu wanaskini ambayo wameanziisha kitaifa kwa ajili ya kutoa fidia kwa sababu ya watu wengine kushindwa kulipa fidia.
Omar Mohamed Ali ni Mkuu wa Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii katika Wizara ya Maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na watoto Pemba alifahamisha kuwa Fidia nikitu ambacho kimetajwa katika sheria.
“Hakimu anapotoa hukumu yake mtendaji amethibitishwa kosa hivyo atatumikia kifungo na pia atatoa fidia kwa muhanga lakini kumekuwa na tatizo mtu akeshafungwa halipi ile fidia”Alifafanua Omar.
Alifahamisha hii ni changamoto ambayo kesi nyingi wanazozipokea ofisini kwao ,wahanga kulalamika kuwa fidia imetajwa katika hukumu hakini hawapati haki yao na ili waipate nilazima wakafungue kesi ya madai .
Aidha Mkuu huyo wa idara alisema kwa mawazo yake binafsi anaona kuwa muhanga atakapopokea fidia akaitumia anahisi itazidi kumuathiri kwani inaweza kupelekea kukumbuka lile tukio kila atakapona kitu alichonunua kupitia fidia ile.
“Hayo ni mawazo yangu binafsi kwa upande wangu nahisi mtu anapopelaka kesi yake mahkamani na ikapata hukumu inatosha kupata haki ile”Alifafanua Omar.
Alisema Iwapo mtu atakuwa anahisi fidia ndio itakayompa haki na utulivu na nafsi yake ,pindi anapokosa fidia baada ya kuhumu basi anahaki kubwa ya kufungua kesi ya Madai na kupelekea kupata fidia yake .
Takwimu za makossa ya udhalilishaji kutoka Afisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar kuanzia Julai mpaka Septemba, 2023 ni kwamba watu 24 wamekutwa na hatia mahakamani kwa kufanya makosa ya udhalilishaji na kupewa adhabu za vifungo ambapo asilimia 58.3 ni vijana wa umri wa 18-29.
Takwimu hizo pia zinaonesha watu ambao bado wapo mahabusu kesi zao zinaendelea ni 48 ambapo kundi hilo la miaka 18 hadi 29 pia linaongoza ambalo linafanya asilimia 54.
Takwimu pia zinaonesha kuwa masuala hayo ya udhalilishaji yanawaathiri watoto zaidi ambapo katika matukio 157 kwa mwezi Julai hadi Septemba yaliyoripotiwa, watoto ni 122 sawa na asilimia 77.
Kwa Muktadha huo basi,Mwandishi wa Makala haya akaamua kuifikia Jamii na kutaka kufahamu ni yepi mawazo yao kuhusiana na ukosekanaji wa fidia ya kesi hizo inavosokota mioyo ya wahanga.
Bi Huda Mohd ni mwananchi na mkaazi wa makondeko Chake chake Pemba alilezea kuwa Ukoseshwaji wa fidia kwa wahanga kunapelekea changamoto kubwa ya watu kumalizana majumbani zinapotokea kesi hizo.
Alifafanua kuwa pamoja na jamii kuelimishwa kuripoti vitendo vya udhalilishaji vinapotokea , imekuwa ngumu kwa baadhi ya wanajamii kuripoti kutokana na kutolipwa fidia .
“Hapo huamua kukaa familia zote mbili majumbani mwao na kulipana kama fedha au vitu vya thamani ,ili kulipia fidia kwa muhanga wa matendo hayo”Alifafanua.
Aidha alifahamisha kuwa kuna umuhimu wa serikali kuliangalia kwa umakini masula haya ya ulipaji wa Fidia kwa wahanga ,kufanya hivyo kutapelekea wahanga kuripoti kesi hizo na kuacha kabisa masuala ya kuishia suluhu majumbani mwao.
Kwa Upande wake Munira Ali Masoud Mkaazi wa Jadida Wete Pemba alilezea kuwa kutolipwa kwa fidia kwa wahanga kunapelekea athari nyingi ikiwemo ,muhanga kuona kuwa hajapata ile haki anayostahili kuipata .
Aidha alisema kuwa Sio kama wahanga wote watafarijika na kusahau ule mtihani waliopata lakini waliowengi kwa mawazo yake watafarajika.
Kwa Upande wake Ghalib Mohamed Mkaazi wa Machomane Chake Chake Pemba alihamisha kuwa fidia ni kitu cha lazima kwa wahanga ,kwa kupunguza machungu pamoja na kuleta Imani na vyombo husika vya sheria.
Alitoa ushauri kuwe na Mahkama maalum za makosa ya udhalilishaji ambayo inatenda haki katika maamuzi kwa pande zote mbili ,mtuhumiwa atakopothibiti na ushahidi ukapatikana anahatia basi na fidia itoke muda uleule atakapoanza kifungo chake .
“Atakapofanyiwa udhalilishaji wa ubakaji mtoto , mtuhumiwa akafungwa miaka15 bila fidia haileti maana ,yule muhanga aliyedhalilishwa inakuwa hanaanalolipata zaidi ya matatizo”Alisema Ghalib.
Alisema kuwa ndipo pale inatokea kesi hizo mara nyingi zinakosa mashahidi sababu watu watahisi kama kupoteza muda wao,hivyo fidia nikitu cha lazima na kinaponza machungu.
Hapa sasa ndipo unakuja ule msemo usemao Adhabu ya kaburi aijuae maiti,Mama mzazi wa mtoto aliefanyiwa udhalilishaji anazungumza na mwandishi wa Makala hii alisema Fidia ni muhimu kupatiwa wahanga.
Alieleza kuwa mtoto wake tangu afanyiwe ubakaji ameathirika kimwili na kiakili,na gharama kubwa ya matibabu anapoteza tangu utokee mtihani huo .
“Fidia inapotolewa sio kama inakuja kumfariji tu muhanga bali pia inakuja kumsiadia kulipia zile gharama alizotumia za matatibabu na kufatilia mambo mengine”Alifahamisha.
Alishukuru Mahkama kwa kusimamia vyema kesi hizo pamoja na kuzitolea hukumu ,hivyo aliomba pia kuchukuliwa jitihada kubwa kusimamia fidia ziweze kutolewa kwa wahanga.
Kwa Upande mwengine Baba mzazi wa muhanga mwengine wa makosa hayo ya udhalilishaji alilalamikia kukosa kwa fidia ya milioni 5 tangu ilipotoka hukumu 2020 mpka leo.
Alifahamisha hukumu ilitolewa na mtuhumiwa alifungwa miaka 14 jela na faini ya shilingi milioni 5 kama fidia ya kuyweza kumkimu yule mtoto aliyefanyiwa udhalilishaji.
“Nimefatilia kupata haki yangu hio kwa kipindi kirefu sasa na nimefungua kesi za madai ,na mtuhumiwa alichojibu nikuwa yupo tayari kuengezwa miaka mengine kwani hana uwezo wa milioni 5 “Alifafanua.
Kutokana na kauli ya Baba huyo inaturudisha nyuma mpaka kwa kaimu mwanasheria Dhamana alipozungumzia kuwa sababu kubwa ya kukosekana kwa watuhumiwa hawalipi fidia kutokana na uwezo wao kiuchumi .
Pamoja na hayo Jitihada bado inahitajika katika kulisimamia suala la fidia kutoka kwa wakati ,kufanya hivyo kutapelekea watu kuripoti Kesi za udhalilishaji sehemu husika na sio kuishia suluhu majumbani mwao.
Wazazi na walezi tunatakiwa tuchukue jitihada kubwa katika kusimamia malezi ya watoto wetu,huku tukiwapa elimu za stadi za maisha vijana na kuweza kujiepusha na matendo haya ya udhalilishaji.
MWISHO.