Monday, March 4

HABARI PICHA: TRA yawakabidhi zawadi walipaji bora wa kodi Pemba.

NAIBU Waziri wa Fedha wa Sherikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Hamad Hassa Chande, akimkabidhi zawadi ya mlipaji bora wa kodi mwakilishi kutoka kampuni ya Mafuta ya GAPCO Pemba Makubi, wakati wa hafla ya kilele cha sherehe ya wiki ya shukurani kwa mlipa kodi mwaka wafedha 2022/2023 Pemba
AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba Abdullwahabi Said Bakar, akimkabidhi cheti mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, baada ya Wilaya hiyo kuibuka mshindi wa pili kwa taasisi zinazosaidia kuunga mkono ukusanyaji wakodi mwaka wa fedha 2022/2023, wakati wa hafla ya kilele cha sherehe ya wiki ya shukurani kwa mlipa kodi
NAIBU waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Hassan Chande, akila keki mara baada ya kuihitimisha kilele cha sherehe ya wiki ya shukuran kwa mlipa kodi, kwa mkoa wa kikodi Pemba wakati wa hafla ya kilele cha sherehe ya wiki ya shukurani kwa mlipa kodi
NAIBU waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Hassan Chande, akizungumza na wananchi, wafanyabishara na viongozi wa serikali katika kilele cha sherehe ya wiki ya shukurani kwa mlipa kodi, kwa mkoa wa kikodi Pemba hafla iliyofanyika mjini Chake Chake
VIONGOZI mbali mbali wa TRA Pemba, Unguja na Meneja wa Benk ya NMB Pemba, wakifuatilia kwa makini hafla ya sherehe za kilele cha wiki ya shukurani kwa mlipa kodi, kwa mkoa wa kikodi Pemba hafla iliyofanyika mjini Chake Chake

 

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)