NA – AMINA AHMED
Pemba: “Sikuwa na fedha,maeneo mengine sikuweza kuyafikia ,Elimu ya uongozi sina Chama kilikosa ya kuniwezesha kifedha na safari yangu kwa mwaka 2020 ikaishia asante kwa kushiriki jambo ambalo halikuwa kusudio langu’’ Amesema Riziki Mgeni.
Wahenga waliosema kuwa ‘’Mkono Mtupu Haurambwi‘’ Wakiwa na maana ya kuwa unapofanyiwa jambo lolote hata kama unahitaji usaidizi basi ni lazima uwe na kitu kidogo cha kuongezea ambacho sio ahsante ya mdomo mtupu,wakaendelea kusema kuwa ‘’Mti Hawendi Bila ya Nyenzo’’ yaani ni lazima upate wasaidizi katika kufika safari yako uliokusudia .
Ndivyo hivyo ambavyo imetokea kwa Riziki Mgeni Juma mzaliwa wa Wilaya Chakechake yenye jumla ya wakaazi 25,201 Wadi ya Vitongoji yenye wakazi 6394 (wanaume) 3,050 na 3,344 (wanawake) ambaye anaamini mkononi wake ungekuwa na kitu angeweza kuviepuka vikwazo vya kisiasa na kuwa mmoja kati ya Diwani wa kuchagulia na wananchi Wadi ya Mtambwe mwaka 2020 na kuwa mtetezi wa changamoto za jamii yake hiyo.
Riziki mwenye umri wa miaka 42,Mkaazi wa Wadi ya Mtambwe yenye wakaazi 16,237 ( wanaume) 80 13 (wanawake) 8,224 mama wa 6 ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema -BAWACHA Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo kwa sasa mwanamke huyo ni Mwenyekiti wa Barza hilo Kanda ya Pemba.‘’ Wanawake tunajitokeza na tuna mwamko sana wa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi lakini kuna vikwazo vinavyotukwaza sisi wanawake kwanza ni uwezeshwaji hatufikii malengo ya kuwa viongozi kwa sababu ya uwezeshwaji na kukosa fedha’’. Amesema Riziki huku akiongeza kuwa ‘’Uwezeshwaji wa kifedha binafsi nilishindwa kuzifikia sehemu zote kunadi sera zangu nikaishia kushika nafasi ya tatu ,naamini maeneo ambayo sikuyafikia ningeliyafikia basi saivi ningelikuwa diwani nawatumikia wana Mtambwe lakini sikuwa na uwezo na sehemu nyengine zilihitaji gharama’’Amemaliza Riziki.
Zanzibar yenye jumla wanawake 974,281 sawa na asilimia 51.6 na wanaume 915,492 sawa 48.4 sensa ya watu na makaazi ya waka 2022 kati ya hao ni asilimia (21.14) sawa na wanawake 71 waliojitokeza kuwania nafasi za udiwani ambapo Chama cha Demockrasia na Maendeleo CHADEMA kilisimamisha wagombea kwa asiliamia 7 kwenye nafasi hiyo.
Ikumbukwe kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC kupitia Sera ya ushiriki wa kijinsia 2015 pamoja na mambo mengine imekuwa na dhamira njema ya kuwahamasisha wanawake kushiriki katika uchaguzi kama wapiga kura na wapigiwa kura .‘’Chama changu kilikosa rasilimali fedha kipindi kilichopita na ikapelelea kukosa zile fedha za kufanyia kampeni kwa hiyo tuliwezeshwa tu kielimu mule mule ndani ya chama sisi wagombea ila sio kwa upana wake ambayo ingekuwa yenye kutusaidia ingawa sio kwa ukubwa” Amesema Rziki.
Amesema ‘’Pia tulitakiwa tushindane kwa sera,hoja , bila kujali itikadi zetu za kisiasa tulitakiwa tujengewe uwezo wa kujitambua kuwa sisi ni kitu kimoja tena ibakie wananchi wenyewe tu tena kuchagua wanawake kwa mujibu wa Sera zetu’’ Amesema Riziki
Omar Nassor ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA amesema kuwa “Chama chetu kimekuwa kikiwasaidia wanawake kutimiza malengo yao ikiwemo kugombea nafasi za uongozi ambapo kuanzia nafasi za ndani ya chama ,sambamba na zile za majimboni jambo ambalo limefanikiwa na kuweza ushiriki wa wagombea wanawake katika nafasi nyingi za majimbo kuanzia udiwani uwakilishi na ubunge walijitokeza’’ Amesema Omar wakati akizungumza na Mwandishi wa Makala hii.
Aisha Abdalla Juma ni Mwanaharakati maswala ya wanawake wenye ulemavu kutoka shirikisho la Jumuiya za watu wenye ulemavu Zanzibar SHIJUWAZA amesema kuwa ipo haja kwa serikali kutoa ruzuku maalum kwa ajili ya wagombea wanawake ambayo itawasaidia kuzikabili changamoto hizo.
”Bila kubagua itikadi wala udogo wa vyama serikali ituangalie kwa upekee sisi wanawake hususan ni wale ambao wnakuwa wakijitolea kuwania nafasi mbali mbali iwawezeshe ruzuku kwa kutambua kuwa kundi hili kwa muda mrefu tumeachwa nyuma katika ushirikishwaji’’ Alisema Aisha Abdalla .
‘’ Ulazima huo wa kuwapata viongozi wanawake unahitaji kupaziwa sauti maalum ambazo zitasaidia kuishawishi Serikali kuweka ulazima wa kisheria hata kwa vyama vidogo ambazo zitasaidia kuwawezesha katika uchaguzi na harakati zake.” Muhammed Suleiman mkaazi Madungu.
Riziki anaiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,wadau wa maendeleo kwa wanawake ikiwemo Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA ZNZ kuendelea kutoa elimu kwa wagombea wanawake sambamba na kuwasapoti ili waendelee kushiriki katika harakati hizo za kutafuta nafasi za uongozi “Kuwaezesha kitaaluma , kifedha pamoja na usalama wao bila kujali tofauti za siasa wala udogo wa vyama vyao walivyo huku akiamini kuwa uwezo na umakini walio nao viongozi wanawake wanapo kuwa viongozi , ni ukombozi wa changamoto za jamii zao “ Amemaliza Riziki.
MWISHO