Monday, January 17

afya

Profesa Mnyaa akabidhi Bati 150, mbao 450 kwa  Ujenzi wa kituo cha Afya Tironi
afya

Profesa Mnyaa akabidhi Bati 150, mbao 450 kwa Ujenzi wa kituo cha Afya Tironi

NA ABDI SULEIMAN. KUKAMILIKA kwa Ujenzi wa kituo cha Afya Tironi jimbo la Mkoani Wilaya ya Mkoani, kitaweza kuwapunguzia usumbufu wa kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani umbali wa kilomita 3.9. Wananchi hulazimika kulipia kiasi ya shilingi 3000-2000 hadi 1500 kwa usafiri wa bodaboda, wakati wa kufuata huduma hiyo ya afya kutoka tironi hadi Hospitali ya Abdalla Mzee. Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi, katika hafala ya kukabidhi Bati 150, mbao 450 zilizogharimu jumla ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mkoani Profesa Makame Mbarawa Mnyaa, hafla iliyofanyika skuli ya Tironi Wilaya ya Mkoani. Mmoja ya wananchi wa Kijiji hicho Rahma Kombo Mohamed, alisema suala la huduma ya afya kijijini kwao ni taatizo kubwa, kwani mtu anapos...
TANZIA: WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA WAFARIKI DUNIA KWA AJALI
afya, Kitaifa

TANZIA: WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MWANZA WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

NA MWANDISHI MAALUM “Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda. Hayo yamebainishwa leo Januari 11, 2022 na Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mwanza. “Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ndugu Gabriel (Mhandisi Robert Gabriel) amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia. Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo,”amefafanua Soko.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Ameweka Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kendwa.
afya

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Ameweka Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Kendwa.

NA ABDI SULEIMAN. WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kassim Majaaliwa Majaaliwa amewataka, wananchi wa Zanzibar kuedelea kudumisha Muungano ,amani na mshikamano miongoni mwao kwa kufanyakazi kwa bidii ili kujikwamua kuchumi. Aliyasema hayo huko katika kijiji cha Kendwa kiwani mkoa wa Kusini Pemba wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi Kituo cha Afya , Wodi ya wazazi na Nyumba ya Daktari ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 58 ya Mapinduzi Zanzibar. Alieleza lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuwapunguzia masafa wananchi kwa kuwaletea miundo mbinu ya huduma mbali mbali za kijamii karibu na maeneo yao ikiwemo kuwajengea vituo vya afya ambayo ndi dhamira ya mapinduzi matukufu ya mwaka1964. Aliwataka wananchi wa kisiwa cha Pemba kuendelea kuwaombea duwa vion...
WAZIRI wa Utalii Zanzibar awafariji wahanga wa kuangukiwa na kidungu Pujini
afya, Kitaifa

WAZIRI wa Utalii Zanzibar awafariji wahanga wa kuangukiwa na kidungu Pujini

NA ABDI SULEIMAN WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Muhamed Mussa, amewafariji wananchi na wafanya kazi waliopata ajali ya kuangukiwa na Dungu katika siku ya Utalii duniani mwaka jana. Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inaendelea kuwathamini na kuwajali wananchi hao, ili kuona wanarudi katika hali zao za kawaida. Waziri Lela aliyasema hayo kwa nyakati tafauti, Pujini Dodo, kibaridi na katika ofisi ya kamisheni ya utalii Pemba, alipowafariji wafanyakazi waliopata na mtihani huo. Alisema katika kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi na Mwaka Mmoja wa Wizara hiyo, ameona vizuri kuwajulia hali na kuona maendeleo ya afya zao na kama wapo ambao bado basi Wizara iweze kuwasaidia. “Mimi nimekuja kuwajuulia hali zenu, kuona maendeleo yenu na kama bado Wiza...