Tuesday, October 4

afya

BODABODA WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO  KUJIKINGA NA HIV
afya, ELIMU

BODABODA WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KUJIKINGA NA HIV

NA ABDI SULEIMAN MKUU wa Wlaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, amesema Vijana wa bodaboda na wanamichezo Kisiwnai Pemba, wanapaswa kujikinga na kujilinda dhidi ya maambukizi virusi vya Ukimwi yasiendelee kutokea. Alisema vijana hao shuhuli zao wanazozifanya ni ngumu na wanakutana na mambo mengi, kwani inafika wakati hukubali kulipwa fidia na abiria wao wanaowapakia bila kujali afya zao. Mkuu huyo aliyaeleza hayo alipokua akizungumza na vijana wa bodaboda na wanamichezo, katika bonanza la uhamasishaji na upimaji wa VVU kwa vijana na kufanyika katika viwanja vya Gombani. Aidha aliwataka vijana kuendelea kuchukua tahadhari, ili kuepuka maambukizo mapya ya ukimwi, ili waweze kujenga uwelewa kwao na kuwa wazalishaji wazuri na wanaoweza kufanya kazi vizuri. Akizungumzia ...
MARADHI yasioambukiza yaongoza kuua kimya kimya
afya, ELIMU, Kitaifa

MARADHI yasioambukiza yaongoza kuua kimya kimya

NA ABDI SULEIMAN. WATAALAMU kutoka kitengo cha Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (NCD UNIT), wamesema maradhi hayo yamekuwa ni hatari na kupoteza maisha ya watu kimnya kimnya kuliko maradhi mengine. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani(WHO), zinaonyesha kuwa maradhi hayo yanauwa watu milioni 41 kila mwaka sawa na 71% ya vifo vyote duniani kote mwaka 2021. Hayo yameelezwa na afisa kutoka kitengo hicho Rabia Ali Makame, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari Kisiwani Pemba, katika ukumbi wa maabara ya afya ya jamii Wawi Wilaya ya Chake Chake. Afisa huyo alisema Kila mwaka zaidi ya watu milioni 15 wanakufa kutokana na maradhi yasiyoambukiza, kati ya umri wa miaka 30 mpaka 69 sawa na 85%, ambapo vifo hivo vya mapema hutokea kwa nchi yenye vipato v...
afya, ELIMU

VIDEO: Akinamama wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi wameshauriwa kujiunga na huduma za uzazi wa mpango 

  Na Raya Ahmada. Akinamama wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi wameshauriwa kujiunga na huduma za uzazi wa mpango ili kuepuka kuzaa papo kwa papo ambayo inaweza kupunguza kwa kinga mwilini ambayo inahatarisha kupata magonjwa nyemelezi na hata kumuambukiza mtoto.       Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mratibu wa Tume ya UKIMWI ofisi ya Pemba Ali Mbarouk Omar wakati akizungumza na ZBC ofisini kwake Chake chake.   Amesema akinamama wanapoingia katika huduma hiyo wanapewa ushauri wa kuzaa watoto wanaopishana ili kujipunguzia mzigo wa kupoteza nguvu kwa kujifungua mara kwa mara.   Kwa upande wake Msimamizi wa vituo vya klini za huduma na tiba kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi kanda ya Pemba dk. Rahila Salum Omar amesema mama hao ...
WAFANYA USAFI KUELEKEA SIKU YA USHIRIKA.
afya, Biashara, Kitaifa

WAFANYA USAFI KUELEKEA SIKU YA USHIRIKA.

NA ABDI SULEIMAN. MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, amewataka wananchi wa wilaya wa kisiwa cha Pemba kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya makaazi ili kupunguza maradhi mbali mbali ikiwemo nyemelezi. Mkuu huyo alisema iwapo wananchi watasafisha mazingira katika maeneo yao, wataweza kupunguza hasara kubwa ya maradhi nyemelezi katika maisha ya kawaida, kwani kinga ni bora kuliko tiba. Aidha mkuu huyo aliyaeleza hayo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi wa mazingira, katika barabara ya pangali pondeani, ili ni kuelekea siku ya ushirika duniani. Alisema unapoboresha usafi unaboresha kinga katika maeneo yetu, pamoja na kupunguzia mzigo serikali kutibu, wakati fedha hizo ilizipanga kwa shuhuli nyengine na sio matibabu hayo. “Elimu...
afya, Kitaifa

USHIRIKIANO unahitajika zaidi katika kuhakikisha kunakuwa na ukondoishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu, ili wapate haki zao za msingi.

NA ZUHURA JUMA, PEMBA USHIRIKIANO unahitajika zaidi katika kuhakikisha kunakuwa na ukondoishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu, ili wapate haki zao za msingi. Akiwasilisha mada katika mkutano wa Mtandao wa Wilaya wa Mpango Jumuishi wa Maendeleo katika Jamii (CBID), Mshauri kutoka Shirika la watu wenye ulemavu la Norwey (NAD) Christine Cornick alisema, wamekuwa wakifanya kazi na mtandao huo, ili kuisaidia kuleta mabadiliko katika jamii. Alisema kuwa, ushirikiano wa pamoja ndio utakaoleta nguvu ya kufanya kazi na kuleta mabadiliko ya haraka katika ukondoishaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika nchi mbali mbali. "Katika mtandao huu tumeshirikisha watu mbali mbali, wanakuwa na sehemu ama mahala ambapo wanakutana na kubadilishana uzoefu katika ngazi mbali mbali na kutoa maa...