BAADHI YA WAFANYA BIASHARA HAWAKO TAYARI KUTUMIA MASHINE ZA UTOAJI RISITI. – RC MATAR
(PICHA NA:ABDI SULEIMAN,PEMBA)
BAKAR MUSSA –PEMBA.
MKUU wa mkoa wa Kusini Pemba , Matar Zahor Massoud amesema kuwa pamoja na juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya uhamasishaji wa ulipaji kodi kwa kutumia mashine maalumu za kutolea risiti za Elektronik , lakini bado kuna baadhi ya wafanyabiashara hawajakuwa tayari kuendana na mfumo huo.
Alisema ni wajibu wa kisheria kwa kila Mfanyabiashara kuwa na mashine ya kutolea risiti za Elektronik na kuitumia ili Serikali iweze kupata mapato yake inayostahili na kwa ukamilifu wake.
Matar aliyaeleza hayo huko katika ukumbi wa Mamlaka ya mapato Zanzibar (ZRA) Gombani Pemba wakati alipokuwa akizungumza na Wafanyabiashara wa mkoa wa Kusini kisiwani humo ikiwa ni uendelezo...