Watoto watoro warudishwa skuli
NA ABDI SULEIMAN.
KAMATI ya Kupambana na Vitendo vya Udhalilishaji shehia ya Ndagoni, imeweza kuwarudisha skuli watoto 40 na kujiunga na darasa mbadala, huku 15 kayi yao hawakuwahi kusoma hata darasa la kwanza.
Kamati hiyo imesema watoto 25 waliweza kuacha skuli kutokana na sababu mbali mbali, waliobakia wakianza sasa kusoma baada ya kukosa elimu hapo awali.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia baadhi ya wanafunzi wakiendelea na masomo yao katika skuli hiyo, huku wengi wao wakionekana ni wale waliokatisha kuendelea na masomo huko nyuma.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mratib wa wanawake na watoto shehia ya Ndagoni Wilaya ya Chake Chake, Shuwarika Ali Mohamed, alisema kamati hiyo imeundwa kufuatia kupatiwa elimu na Taasisi ya KUKHAWA Pemba, chini ya mradi wa kata...