Monday, October 18

Kimataifa

Sweden Yamwaga Bilioni 196 Kusaidia Sekta ya Elimu Nchini.
Kimataifa, Kitaifa

Sweden Yamwaga Bilioni 196 Kusaidia Sekta ya Elimu Nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg, wakisaini mkataba wa msaada wa shilingi bilioni 195.9 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR II), jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg, wakibadilishana mkataba wa msaada wa shilingi bilioni 195.9 kwa ajili ya Awamu ya Pili ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR II) baada ya kusainiwa jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto) akipeana mkono na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg, baada ya kusainiwa mkataba wa msaada wa shili...
Unaelewa nini kuhusu fedha kwa kukabili mabadiliko ya tabianchi?
Kimataifa, Kitaifa

Unaelewa nini kuhusu fedha kwa kukabili mabadiliko ya tabianchi?

WMO/Chunseong Bang Juhudi za pamoja za kusaidia kupunguza uchafuzi wa tabaka la ozoni zitafanya tabaka hilo lipone kutokana na majeraha ya uchafuzi kwa miongo kadhaa 20 Septemba 2021 Je unaposikia nchi zilizoendelea zinahamasishwa kutoa fedha kufanikisha miradi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi unaelewa nini?. Je ni nani anasimamia fedha hizo, zinatumika kwenye maeneo gani? nani ananufaika na fedha hizo na uamuzi wa kuanza kuchanga ulitokea wapi? Ufadhili kwa miradi ya tabianchi Fedha za miradi ya tabianchi ni fedha zinazotolewa na watu binafsi, taifa au mataifa ambazo zinakusanywa kutoka vyanzo vya umma, binafsi na vyombo mbadala kwa lengo la kusaidia hatua za kupunguza na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. ...
RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA NEW YORK MAREKANI
Kimataifa

RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA NEW YORK MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 22 Septemba, 2021 ameshiriki mkutano wa pamoja kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani na kuhimiza kuimarishwa kwa biashara kati ya mataifa hayo mawili ili kuwa na faida kwa pande zote. Mhe. Rais Samia amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa kwa sasa biashara zinazofanyika kati ya Tanzania na Marekani ni ndogo ikilinganishwa na fursa zilizopo. Amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019, Tanzania iliagiza bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 241na kuuza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 46. Kwa upande mwingine Marekani imewekeza Tanzania Dola za Kimarekani bilioni 5.55 na kuajiri watu 44,118 wakati Tanzania imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja tu ambacho ni k...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Azungumza na Jukwaa la Wafanya Biashara Kati ya Tanzania na Marekani.
Kimataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Azungumza na Jukwaa la Wafanya Biashara Kati ya Tanzania na Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye mkutano wa pamoja kati ya Wafanya Biashara wa  Tanzania na Marekani ambapo amesisitiza kuimarishwa kwa Biashara kati ya Mataifa hayo mawili ili kuwa na faida kwa pande zote mbili. Mkutano huo umefanyika Jijini New York Nchini Marekani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye mkutano wa pamoja kati ya Wafanya Biashara wa  Tanzania na Marekani ambapo amesisitiza kuimarishwa kwa Biashara kati ya Mataifa hayo mawili ili kuwa na faida kwa pande zote mbili. Mkutano huo umefanyika  leo Sept 22,2021 Jijini New York Nchini Marekani.