Thursday, August 11

MAZINGIRA

Serikali itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza miradi  ya kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.
Kitaifa, MAZINGIRA

Serikali itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza miradi ya kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Serikali imesema itaendelea kutafuta fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa pande zote mbili za Muungano. Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini – EBARR unaotekelezwa katika Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja na kusimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Akiwa katika eneo la Mbuyutende Dkt. Mkama ametoa rai kwa wanufaika wa mradi wa boti (6) za uvuvi zilizotolewa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kutumia boti hizo katika shughuli za uvivu na utalii kama shughuli mbadala ya kujio...
MAZINGIRA

JET yawakutanisha wahariri tanzania kujadili masuala ya uhifadhi

        NA ABDI SULEIMAN.   CHAMA cha waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET), kinatarajia kuwakutanisha wahariri wa Habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini, kwa lengo la kuwaongeza uwelewa juu ya masuala uhifadhi wa korido katika maeneo yanayounganisha wanyamapori, uhifadhi wa baharini na misitu, usafirishaji na ujangil, kukuza uhifadhi wa wanyamapori na utalii.   JET imesema kuwa jumala ya wahariri 25 kutoka vyombo mbali mbali vya habari, wataweza kubadilishana uzoefu ili kuweza kuzihakiki kwa uzuri habari zinazochapishwa na waandishi wao habari wanaoshiriki katika program za mafunzo kutoka JET.   Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa JET John Chikomo, alisema mkutano huo wa mashauriano na wahariri wa habari, uta...
Biashara, Kitaifa, MAZINGIRA, Utamaduni

SERIKALI kupitia Wizara ya Utalii Zanzibar imeanza kuyafanyia ukarabati majengo ya kihistoria kwa lengo la kurejesha uasili wake.

NA ZUHURA JUMA, PEMBA SERIKALI kupitia Wizara ya Utalii Zanzibar imeanza kuyafanyia ukarabati majengo ya kihistoria kwa lengo la kurejesha uasili wake, jambo ambalo litasaidia kuimarisha utalii kisiwani Pemba. Akizungumza Chwaka Tumbe Wilaya ya Micheweni, Matibu wa Idara ya Makumbusho Pemba Khamis Ali Juma alisema kuwa, majengo ya kihistoria yamekuja na sura mpya ya utalii, hivyo yakifanyiwa maboresho yatarudi katika uasili wake. Alisema kuwa, Idara yao ina dhamira ya kurejesha uasili wa majengo ya kihistori kwa lengo la kuimarisha utalii na kurudisha historia kamili, ili vizaji vijavyo viweze kujua. “Tunafanya ukarabati lakini tunafuata vile vile yalivyo majengo haya na tunatumia zana zile zile, ili yawepo katika uasili wake, hivyo tunaamini kwamba wataimarisha utalii kwani ma...
WAKULIMA wa Viungo 666 wa mradi wa viungo na mboga mboga wakabidhiwa vifaa
Biashara, Kitaifa, MAZINGIRA

WAKULIMA wa Viungo 666 wa mradi wa viungo na mboga mboga wakabidhiwa vifaa

Na Gaspary Charles - TAMWA ZNZ JUMLA ya vifaa 11, 000 vya kuhifadhia mazao ya Viungo na Mboga mboga vimetolewa kwa wakulima 666 wanufaika wa Mradi wa Viungo, Mboga na Matunda kisiwani Pemba unaotekelezwa kwa mashirikiano ya taasisi za People’s Development Forums (PDF), Community Forests Pemba (CFP) na Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya chini ya mpango wa AGRI-CONNECT Tanzania. Utolewaji wa vifaa hivyo ambao ni sehemu ya utekelezaji mradi huo katika kufungua mnyororo wa thamani kwa wakulima wa mazao hayo Zanzibar unalenga kuwawezesha wakulima kukabiliana na tatizo la upotevu na uharibifu wa mazao ya chakula unaosababishwa na wakulima kukosa mbinu na zana bora za kuhifadhia mazao wakati na baada ya mavuno. Mion...