Sunday, March 26

Michezo

YANGA SC YAICHAPA IHEFU FC 1-0, YAKICHIMBIA KILELENI
Michezo

YANGA SC YAICHAPA IHEFU FC 1-0, YAKICHIMBIA KILELENI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM KLABU ya Yanga Sc imefanikiwa kulipa kisasi kwa kuichapa Ihefu Fc kwa bao 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.. Katika mchezo huo, tumeshuhudia mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Kalala Mayele ameweza kuongeza kalama yake ya mabao baada ya kufunga kwenye mechi hiyo. Mchezo wa kwanza mzunguko wa kwanza Yanga iliharibiwa Unbeaten ya 50 na kufikia 49 kwa kufungwa bao 1-0.
RAIS DK. MWINYI AHUDHURIA TAARAB MAALUM YA MIAKA 59 YA MAPINDUZI
Kitaifa, Michezo, Utamaduni

RAIS DK. MWINYI AHUDHURIA TAARAB MAALUM YA MIAKA 59 YA MAPINDUZI

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi jana usiku alijumuika na wananchi na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kwenye taarabu rasmi ya maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo. Taarabu hiyo ilitumbuizwa na vikundi viwili tofauti kikiwemo kikundi cha sanaa cha taifa pamoja na kikundi cha “Island Morden taarabu, maarufu kama Wajelajela” ilikua maalumu kwa kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 pamoja na kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani kipindi cha miaka miwili ya uongozi kwa kuiletea Zanzibar maendeleo makubwa. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar ulipambwa kwa vifijo na hoi...
SMZ Kuifanyia Mageuzi Makubwa Sekta ya Michezo kwa Kujenga Viwanja vya Kisasa – Dk.Mwinyi
Michezo

SMZ Kuifanyia Mageuzi Makubwa Sekta ya Michezo kwa Kujenga Viwanja vya Kisasa – Dk.Mwinyi

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imekusudia kuifanyia mageuzi makubwa sekta ya michezo visiwani kwa kujenga viwanja vya kisasa vinavyoendena na hadhi ya miaka 59 ya Mapinduzi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la viwanja vya michezo, Matumbaku, wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja unaosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, (ZSSF). Dk. Mwinyi aliiagiza bodi ya Mfuko wa ZSSF kuharakisha ujenzi ili ukamilike kwa wakati na wananchi wapate huduma wanazostahiki Aidha, aliiamuru bodi hiyo kuikopesha fedha serikali ili wakamilishe kwa wakati maeneo yote ya ujenzi wa viwanja hivyo vikiwemo viwanja vya mpira wa mikono, (basketball netball, handball na volball) ambavyo vilikua nje ya bajeti n...