Tuesday, April 13

Michezo

SIMBA YAPOTEZA KOMBE LA MAPINDUZI, YANGA YAPETA JUMLAJUMLA
Kitaifa, Michezo

SIMBA YAPOTEZA KOMBE LA MAPINDUZI, YANGA YAPETA JUMLAJUMLA

KIKOSI cha Yanga kimeibuka na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Simba baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana. Nyota wa mchezo huo ni Farouk Shikalo ambaye aliokoa penalti moja ya Joash Onyango na Meddie Kagere kugongengesha mwamba penalti yake moja. Saido Ntibanzokiza ambaye alikuwa msumbufu ndani ya dakika zote 90 amesema kuwa wachezaji wenzake walimuomba awape sapoti naye akasema  kwamba hana tatizo atafanya kazi. Alifunga penalti ya mwisho iliyomshinda mlinda mlango Beno Kakolanya ambaye hakuwa na namna baada ya kuoka hatari tano ndani ya dakika 90. "Ilikuwa sijapangwa kucheza ila wachezaji waliomba nicheze nami nikasema kwamba nitacheza kwa kuwa mchezo ni kazi yangu na nimefanya hivyo ninafurahi. "Mashabiki wangu na m...
RIKODI YAWABEBA SIMBA MAPINDUZI CUP
Michezo

RIKODI YAWABEBA SIMBA MAPINDUZI CUP

  Fainali ya 15 ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuchezwa kesho Jumatano January 13, 2021 kati ya Yanga dhidi ya Simba saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan. Kuelekea katika Fainali hiyo, Abubakar Khatib (Kisandu) Muandishi wa Michezo Zanzibar kuna mambo muhimu unapaswa kuyafahamu kakuandalia:- 1. Yanga ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu mabao machache (1) kuliko Simba ilokubali Nyavu zake kuguswa mara 2, hivyo Safu ya Ulinzi ya Yanga inayoongozwa na Mlinda Mlango Farouk Shikalo na Walinzi wake Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Abdalla Shaibu (Ninja)  na Said Juma (Makapu) inaonekana ndio safu bora mpaka sasa Katika Mashindano hayo. 2. Simba wameingia fainali mara nyingi kuliko timu yoyote (na hii itakuwa mara 8) ambapo Yanga ndo kwanza hii fainali yao ya 3. ...
FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI NI YANGA V SIMBA
Michezo

FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI NI YANGA V SIMBA

  MABINGWA mara tatu wa Kombe la Mapinduzi Simba wanatinga hatua ya fainali baada ya kushinda mbele ya Namungo FC kwenye nusu fainali ya pili kwa ushindi wa mabao 2-1. Mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Simba ilianza kushinda mapema dakika ya 6 kupitia kwa Meddie Kagere baada ya kiraka, Abdulhaman Humud kujichanganya wakati wa kuokoa hatari. Bao la pili ilikuwa ni kazi ya Miraj Athuman dakika ya 39 baada ya kutumia mpira uliopigwa na kiungo Hassan Dilunga kugonga mwamba akakutana nao ukiwa unarejea uwanjani na kuuzamisha kambani. Namungo hawakuwa wanyonge kipindi cha pili waliwapa tabu Simba ambapo dakika ya 83 Kichuya Shiza aliingia ndani ya uwanja akichukua nafasi ya Jaffary Kibaya. Ilimchukua dakika nne kuweza kutengeneza nafasi ambapo alitoa pasi kwa kupi...
SIMBA YATEMBEZA 4G KIMATAIFA, WIDA YAKUBALI KWA WAZIMBABWE
Michezo

SIMBA YATEMBEZA 4G KIMATAIFA, WIDA YAKUBALI KWA WAZIMBABWE

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Januari 6 kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba imepata matokeo hayo ikiwa nyumbani na kufanikiwa kupindua meza kibabe baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kufungwa bao 1-0. Bao la kwanza, Uwanja wa Mkapa lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 39 kwa mkwaju wa penalti baada ya Shomari Kapombe kuchezewa faulo ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti. Licha ya wachezaji wa FC Platinum kuonekana wakilalamika mwamuzi aliamuru ipigwe penalti na bao la pili lilifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 62. Bao la tatu ilikuwa ni John Bocco dk 90+1 na msumari wa nne ni Clatous Chama kwa penalti dakika ya 90+5 na kuif...
KOCHA Cedric Kaze ataja sababu ya kupata sare na Timu ya Jamhuri
Michezo

KOCHA Cedric Kaze ataja sababu ya kupata sare na Timu ya Jamhuri

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Yanga Cedric Kaze amesema wachezaji ambao wamo katika kikosi chake wana uwezo wa kutosha wa kucheza mashindano ya kombe la Mapinduzi. Kocha huyo aliyaeleza hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati yake na Jamhuri ambao walitoka sare tasa, hali iliyoonekana kwamba matokeo hayo yametokea kutokana na kuwakosa baadhi ya wachezaji wake. Alisema kuwa kilichofanyika katika kikosi cha chake ni maamuzi ya ufundi kutokana na wachezaji hao kutumika sana katika mechi za ligi na iliwapasa wapumzike. “Wachezaji wametumika sana kwenye ligi tunatoka kwenye ziara ya mikoani na siku 21 tumeishi njiani na tulicheza mechi nne sasa kuna wachezaji wengine wamechoka sana na mechi za ligi na kutokana na mwili wa mchezaji ilibidi apumzike”, alisema. Hivyo alisema kuwa anaam...