KIKUNDI cha mazoezi cha Mtu ni Afya Fitness Club cha Kidike kutembea shehia hadi shehia, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi
KIKUNDI cha mazoezi cha Mtu ni Afya Fitness Club cha Kidike, kimesema kinakusidia kutembea shehia hadi shehia, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi, ili kuwatayarisha vijana kushiriki katika michezo mbali mbali.
Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Kojani Hamad Hassan Chande, baada ya kumaliza matembezi yalioanzia Mchangamdogo hadi Madenjani na ufanyaji wa mazoezi ya Viungo, pamoja na kukabidhi Jezi na Fedha taslimu kwa ajili ya bonanza la michezo linalotarajiwa kufanyika Januari Mosi 2021.
Alisema kupitia vikundi hivyo anaamini kwamba upo uwezekano mkubwa wa kuibua vipaji mbali mbali vya michezo, ikiwemo mchezo Riadha, mpira wa miguu na resi za baskeli, ambapo watakua na uwezo wa kushiriki michezo mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.
Aliwa...