Kesi 61 za madawa ya kulevya kuanzia Januari 2019 hadi Disemba 2020 zaripotiwa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba.
NA ZUHURA JUMA, PEMBA
JUMLA ya kesi 61 za madawa ya kulevya zimeripotiwa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, kuanzia Januari 2019 hadi Disemba 2020.
Kesi hizo za madawa ya kulevya ambayo ni bangi na unga aina ya heroin, mwaka 2019 ziliripotiwa 28 na mwaka 2020 ziliripotiwa kesi 33.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis alisema, wataendelea kupambana ili kuhakikisha madawa ya kulevya hayaingizwi katika mkoa huo.
Alisema kuwa, Jeshi hilo linaendelea kuwaonya wananchi wanaojihusisha na uuzaji, uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya na kwamba halitomvumilia mtu yeyote atakae bainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Alieleza kuwa, ni kosa kisheria kuingiza, kuuza na kutumia dawa za kulevya, hivyo atakaebainika kujihusis...