Friday, April 23

Sheria

MTOTO mmoja mchanga amekutikana  ndani ya sinki la choo cha hospitali ya Chake chake Pemba
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

MTOTO mmoja mchanga amekutikana ndani ya sinki la choo cha hospitali ya Chake chake Pemba

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA MTOTO mmoja mchanga, anaekisiwa kuzaliwa kwa miezi saba, amekutikana ameshafariki dunia, ndani ya sinki la choo cha hospitali ya Chake chake Pemba, huku mama aliyemzaa mtoto huyo, akiwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kusini Pemba. Mwandishi wetu ambae alifika hospitali ya Chake chake, alimshuhudia mtoto huyo akiwa ndani ya sinki hilo, kwenye choo kinachotumiwa na wagonjwa wanawake, wanaofika hospitalini hapo. Akizungumza na mwanadishi wa habari hizi, kwenye eneo la tukio, Daktari dhamana wa hospitali ya Chake Chake Ali Omar Khalifa, alisema mtoto huyo, aligundulika majira ya saa 3:00 asubuhi. Alisema tukio hilo, linaonekana kufanyika baina ya saa 1:00 asubuhi ya Januari 9 mwaka huu, wakati mmoja wa wagonjwa waliofika hospi...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi atoa msamaha kwa wanafunzi (wafungwa) Arobaini na Tisa (49) waliokuwa Vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba
Kitaifa, Sheria

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi atoa msamaha kwa wanafunzi (wafungwa) Arobaini na Tisa (49) waliokuwa Vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa msamaha kwa wanafunzi (wafungwa) Arobaini na Tisa (49) waliokuwa wakitumikia Vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Sherehe za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Dk. Mwinyi ametoa msamaha huo kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kinachompa mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa waliofungwa gerezani. Kutokana na msamaha huo, Dk. Mwinyi ameamuru kuwa kifungo kilichobaki cha wanafunzi (wafungwa) hao walionufaika na msamaha katika vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba kuwa kipindi hicho chote kinafutwa na waachiwe huru kuanzia Januari 11.2021. Kwa vile,  Zanzibar itakuwa inasherehekea miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Janu...
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesaini makubaliano ya kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania
Kitaifa, Sheria

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesaini makubaliano ya kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania

  DODOMA, 23/12/2020 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesaini makubaliano ya kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania kwa lengo la kupanua wigo wa kuelimisha jamii na chama hicho kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na majanga, makubaliano hayo yamefanyika Jijini Dodoma mapema leo asubuhi. Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Skauti Mkuu, Mwantumu Mahiza alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa wimbi la moto kwenye shule na katika jamii. “Kazi ya chama cha Skauti ni kusaidia watu na viumbe na kuhakikisha nchi inakuwa na amani na salama kwa kuishi. Tulipoona majanga ya moto yanajitokeza kwenye shule na makazi ya watu, Skauti tukaona kuna haja ya kushirikiana na chombo cha kisheria. “Skauti tumeshiriki kwenye mambo mengi ya Uokoaji, tulikuwa tunafa...
Jamii iendelee  kudumisha amani na utulivu nchini.
Kitaifa, Sheria

Jamii iendelee kudumisha amani na utulivu nchini.

  WADAU wa uchaguzi Kisiwani Pemba wametakiwa kuishajihisha jamii kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini katika kipindi hichi ambacho Taifa linatoka katika uchaguzi mkuu. Uchaguzi umemaliza na serikali iko madarakani hivyo lililopo kwa sasa ni kudumisha amani na utulivu na kusahau yaliyopita kwani ukizingatia kuna maisha baada ya uchaguzi. Akitowa mada juu  umuhimu wa kulinda amani kwa wadau hao uliofanyika ukumbi wa Maktaba Chake chake kaimu mratibu wa kituo cha huduma za sheria tawi a Pemba Safia Saleh Sultan alisema kila mmoja ana haki ya kulinda amani na kuondosha ugomvi ,vita na mifarakano katika nchi ili kila mmoja aweze kuendesha maisha kwa salama . Alifahamisha kuwa ili amani iweze kudumu vyema ni vizuri kuanzia ndani ya familia na baadae kwenye shehia, wi...
Ahukumiwa kwenda chuo cha mafunzo.
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Ahukumiwa kwenda chuo cha mafunzo.

  Kijana  Khamis  Shaib Khatib  mwenye umri wa miaka  24 mkaazi  wa Kizimbani Wete Pemba ahukumiwa kwenda  chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka  saba  [7]  na kutozwa faini ya shilingi laki mbili za kitanzania baada   ya  kupatikana na hatia ya kumbaka  msichana wa miaka kumi na tatu [13]. Hukumu hiyo imesomwa na  hakimu  Abdala  Yahya  Shamuhun  baada  ya kuona ushahidi uliotolewa mahakamani hapo unaridhisha. Hakimu huyo alimtaka mshitakiwa huyo kwenda kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka  saba [7] na kutozwa fidia ya shilingi laki mbili baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kubaka. “Mtuhumiwa umepatikana na hatia kwa  kosa la  kubaka  utatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka  saba[7]” alisema shamuhun. Kabla ya kusomewa shitaka lake hilo mshitaki...