Friday, August 12

vijana

TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na NED waja na mkakati mpya kuwajengea uwezo wanahabari vijana 18 Z’bar
ELIMU, Kitaifa, vijana, Wanawake & Watoto

TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na NED waja na mkakati mpya kuwajengea uwezo wanahabari vijana 18 Z’bar

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema ili  tuweze kukuza usawa wa kijinsia visiwani Zanzibar kuna ulazima waandishi wa habari kutoa taarifa za wanawake na maendeleo yao katika Nyanja  tofauti zikiwemo za uongozi, na maendeleo ya kijamii. (more…)
DC CHAKE CHAKE AZINDUA HUDUMA YA TELEZA KIDIJITALI
Biashara, Kitaifa, vijana, Wanawake & Watoto

DC CHAKE CHAKE AZINDUA HUDUMA YA TELEZA KIDIJITALI

NA ABDI SULEIMAN MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, ameishukuru benk ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono juhudi mbali mbali za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ya kuwasaidia vijana wasio na ajira katika suala zima la kujiajiri wenyewe na kukuza kipato kwa walionacho. Alisema ili kujikomboa katika uchumi na changamoto walizonazo vijana, kufungua akaunti katika benk ya NMB kwani wataweza kunufaika na huduma mbali mbali zinazotolewa na benk hiyo. Mkuu huyo wa wilaya aliyaeleza hayo wakati wa uzinduzi wa huduma ya TELEZA KIDIJITALI, kwa wananchi wa Wilaya ya Chake Chake na wafanyabiashara, halfa iliyofanyika katika soko la matunda Chake Chake, chini ya benk ya NMB Tawi la Pemba. Alisema iwapo watafungua akaunti katika benk hiyo, wataweza kujikomboa kiuchum...
WATAKIA kuepuka kujiingiza katika makundi hatarishi vijana
ELIMU, Kitaifa, vijana

WATAKIA kuepuka kujiingiza katika makundi hatarishi vijana

NA ABDI SULEIMAN. WANANCHI wa shehia ya Wawi Wilaya ya Chake Chake, wametakiwa kufuatilia mienendo ya vijana wao, ili kuepuka kujiingiza katika tabia hatarishi ambazo zinaweza kuwapelekea kubaya. Hayo yameelezwa na kaimu mratibu Tume ya Ukimwi Zanzibar Ofisi ya Pemba, Ali Mbarouk Omar katika mkutano wa uhamasishaji jamii juu ya masuala ya Tabia hatarishi, mkutano uliofanyika Wawi. Alisema iwapo wazazi watakua makini na vijana wao, matukio maovu yanaweza kupungua na hata kujiingiza katika vikundi hivyo na kuepuka kuiga tabia hatarishi. Aidha kaimu huyo aliwataka Vijana kujitahidi kuchunguza afya zao hospitali, kwa kuangalia maradhi mbali mbali ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. “Shehia hii imekua na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbali mbali, tabia zinabadilika...
Wajane ni sehemu ya jamii hawapaswi kusahaulika-MAMA MARYAMU MWINYI
Kitaifa, vijana, Wanawake & Watoto

Wajane ni sehemu ya jamii hawapaswi kusahaulika-MAMA MARYAMU MWINYI

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Maryam Mwinyi amesema kundi la wajane ni sehemu ya jamii lilosahaulika sana na kulifanya kukosa haki zake. Mama Maryam aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Riziki Pembe Juma katika maadhimisho ya siku ya wajane duniani katika ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni. Alisema kutokuwepo kwa takwimu sahihi za wajane na kukosa msukumo wa kuzifanyia kazi Tafiti hizo nchini ni moja ya changamoto. Aidha alisema hali hiyo inasahabisha suala la wajane kuwa lisiloeleweka na kutambulika bayana katika Jamii kubwa zinazoishi na makundi hayo. Mama Maryam alibainisha kuwa hilo linadhihirisha na ukweli kuwa vitendo vya unyanyasaji na ...
SEKONDARI kiwani yashinda mashindano ya ukimwi
afya, ELIMU, Kitaifa, vijana

SEKONDARI kiwani yashinda mashindano ya ukimwi

NA ABDI SULEIMAN. SKULI ya sekondari Kiwani Imefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza kwa kupata asilimia 70%, katika mashindano ya chemsha bongo ya Ukimwi, mashindano hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), yakiwa na lengo la kutoa uwelewa kwa wanafunzi juu ya masuala mbali mbali ya VVU na Ukimwi. Nafasi ya Pili ikachukuliwa na skuli ya Amini Sekondari kutoka Wesha iliyopata 66%, nafasi ya tatau ikaenda kwa skuli ya Chwale Sekondari iliyopata alama 63%, nafasi ya nne ikiwenda kwa skuli ya Shumba Sekondari, Uwandani sekondari nafasi ya tano na sita ikaenda kwa skuli ya Mwitani Sekondari. akizungumza na wanafunzi hao Mjini Chake Chake, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Ahmed Aboubakar, aliwataka walimu kuziimarisha klabu za UKIMWI katika skuli zao, ili...