UNESCO, TAMWA-ZNZ yasaini makubaliano kupambana na udhalilishaji ZNZ.
Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanazibar) zimesaini mkataba wa mradi kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mradi huo wa miezi mitatu wenye thamani ya dola za Marekani 17,000, umesainiwa kati ya Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar, Dk. Mzuri Issa Ali na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Michael Toto, katika hafla iliyofanyika Tunguu Wilaya ya kati Unguja.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Mzuri alisema mradi huo utaongeza nguvu mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto ambayo ni moja ya mikakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais, Dk. H...