Tuhuma za kutorosha na kubaka bado zamsotesha rumande.
Mtuhumiwa Bakar Mbwana Juma mwenye umri wa miaka 32 mkaazi wa Jomvu Kengeja anaekabiliwa na shitaka la Kumtorosha na Kumbaka msichana mwenye umri wa 17 ameiambia mahakama ya Mkoa Chake Chake kuwa yeye hahusiki na tukio hilo kwani muda uliotajwa kutenda kosa hilo alikua kwenye kibanda akinywa kahawa.
Aliambia mahakama hiyo kuwa yeye ni mfanya kazi wa ujenzi wa nyumba hivyo anakawaida ya kurudi kazini baina ya saa moja hadi saa moja na nusu za usiku na mara zote hufikia kwenye mkahawa kabla ya kwenda anakoishi.
Alidai kuwa siku ambayo alituhumiwa kufanya tukio hilo alirudi kazini majira ya moja za usiku na kifikia mgahawani na kupata kahawa akiwa yeye na marafiki zake.
Alifahamisha kuwa baada ya kunywa kahawa alirudi nyumbani na kuigia chooni kwa ajili kujiandaa na sa...