WAKULIMA wa Viungo 666 wa mradi wa viungo na mboga mboga wakabidhiwa vifaa
Na Gaspary Charles - TAMWA ZNZ
JUMLA ya vifaa 11, 000 vya kuhifadhia mazao ya Viungo na Mboga mboga vimetolewa kwa wakulima 666 wanufaika wa Mradi wa Viungo, Mboga na Matunda kisiwani Pemba unaotekelezwa kwa mashirikiano ya taasisi za People’s Development Forums (PDF), Community Forests Pemba (CFP) na Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya chini ya mpango wa AGRI-CONNECT Tanzania.
Utolewaji wa vifaa hivyo ambao ni sehemu ya utekelezaji mradi huo katika kufungua mnyororo wa thamani kwa wakulima wa mazao hayo Zanzibar unalenga kuwawezesha wakulima kukabiliana na tatizo la upotevu na uharibifu wa mazao ya chakula unaosababishwa na wakulima kukosa mbinu na zana bora za kuhifadhia mazao wakati na baada ya mavuno.
Mion...