Thursday, September 23
WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba watakiwa  kujua Sera, Katiba, Sheria na vifungu vyake katikautendaji wao wa kazi
Kitaifa

WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba watakiwa kujua Sera, Katiba, Sheria na vifungu vyake katikautendaji wao wa kazi

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kujua Sera, Katiba, Sheria na vifungu vyake ili kuwasaidia kuzitumia katika kuandika habari zao za wanawake kushiriki katika uongozi. Akiwasilisha mada katika mafunzno ya waandishi wa habari juu ya kuwajengea uwezo wanawake kudai haki zao za kisiasa na uongozi, Mwanasheria Mohamed Hassan Ali alisema, kujua vifungu vya Sera, Sheria na katiba ni muhimu sana kwa waandishi. Alisema kuwa, Serikali zote mbili ambayo ni ya Zanzibar na ile ya Tanzania imempa fursa mbali mbali mwanamke, ikiwa ni pamoja kuwa kiongozi, hivyo ni muhimu kwa waandishi kutumia vifungu hivyo wanapoandika habari zao, ili jamii ielewe kwamba wanawake nao wana haki ya kuwa viongozi. "Kwa kweli ni wenyewe tu wanawake hawajaamua au tu...
MHE. HEMED: SMZ INATAMBUA MCHANGO WA INDIA KATIKA HUDUMA ZA UTABIBU
afya

MHE. HEMED: SMZ INATAMBUA MCHANGO WA INDIA KATIKA HUDUMA ZA UTABIBU

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na India katika  sekta ya Utabibu kwa kuimarisha Afya za wananchi wake. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameleza hayo wakati akizungumza na viongozi wa hospital ya SIMS ya India Afisni kwake Vuga jijini Zanzibar. Amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na hospitali hiyo kutokana na matibabu mazuri yanayotolewa na madktari katika nyanja mbali mbali akitolea mfano magongwa ya moyo, saratani,tenzi dume na magonjwa mengineyo. Nae, Mkurugenzi Mkuu kutoka hospital ya SIMS Bw. Galal Ahmed Dawood amemshkuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa ushirikiano wanaopatiwa kutoka serikalini  tangu hospital yao ilipoanza kufanya kazi  zake. Kwa upand...
NAIBU WAZIRI KATAMBI ATAKA WAAJIRI KUZINGATIA SHERIA ZA KAZI KATIKA MAENEO YAO YA KAZI
Kitaifa

NAIBU WAZIRI KATAMBI ATAKA WAAJIRI KUZINGATIA SHERIA ZA KAZI KATIKA MAENEO YAO YA KAZI

Na: Mwandishi Wetu WAAJIRI na wamiliki wa makampuni wameaswa kuzingatia sheria za kazi katika maeneo yao ya kazi ili waweze kuboresha mazingira ya utendaji kazi utakaoleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi. Kauli hiyo ametolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga alipotembelea Mgodi wa almasi wa Al – Hilal Mineral Ltd uliopo wilayani Kishapu na Kiwanda cha Jielong Holding kilichopo Shinyanga Mjini kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sheria za kazi kwenye maeneo mbalimbali ya kazi. Naibu Waziri Katambi alisema kuwa ni wajibu wa waajiri kuhakikisha wanatekeleza sheria za kazi katika maeneo ya kazi akitolea mfano wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya...
Wanafunzi Wote Waliokuwa Hawakuhudhuria Shule Kuanzia 1 Marchi 2021 Kuazia Shule za Msingi na Sekondari Wazazi Wao Kuchukuliwa Hatua.
Kitaifa

Wanafunzi Wote Waliokuwa Hawakuhudhuria Shule Kuanzia 1 Marchi 2021 Kuazia Shule za Msingi na Sekondari Wazazi Wao Kuchukuliwa Hatua.

  Na Hamida Kamchalla, HANDENI. KUFUATIA kitendo cha  wanafunzi 25 wa kata ya Malezi waliomaliza darasa la saba na kufaulu kuingia kidato cha kwanza kutohudhuria masomo kuanzia januari mwaka huu, onyo kali limetolewa kuhusu Mtendaji wa kata hiyo pamoja na wazazi. Wazazi wa kata hiyo wanahusishwa na tuhuma za kuwashawishi na kuwakataza watoto wao kutofanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho kwa lengo la kufeli na kudaiwa kuwaozesha huku Mtendaji wa kata hiyo akiwa hatou taarifa yoyote juu ya kinachotokea kwa upande wa elimu. Akisoma risala mbele ya Mbunge wa Handeni mji Reuben Kwagilwa, Ofisa Elimu kata hiyo George Silas alisema kutokana na kata hiyo kutokua na shule ya sekondari baadhi ya wazazi wanachukulia changamoto ya umbali wa kufuata shule kata ya Kwenjug...