Sunday, August 1
Wizara yakabidhi vifaa vya ushoni kwa vijana.
Kitaifa

Wizara yakabidhi vifaa vya ushoni kwa vijana.

WIZARA ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, imekabidhi vifaa mbali mbali vya ushoni kwa viongozi wa Wilaya nne za Pemba, kwa ajili ya vijana waliomaliza mafunzo ya ushoni Kisiwani hapa, kwa lengo la kuendelea ujuzi wao huo pamoja na kujikwamua na umasikini. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni pamoja na vyarahani 76 Butterfly na Sinja, overlock 12, Pasi 20, Mikasi 123, trpu 72 na Juki 12 ili kuwasaidia vijana hao kufikia malengo yao ikiwemo kushona bila ya usumbufu. Akitoa maelezo juu ya utoaji wa msaada huo kwa vijana, afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, alisema utoaji wa mssada huo kwa vijana umetokana na mipango madhubuti ya Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Shein, katika kuwasaidia vijana wa Zanzibar kupitia program ya vijana. Al...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi awasili Dodoma kuhudhuria ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kitaifa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi awasili Dodoma kuhudhuria ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyiamewasili Jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dk. Hussein amepokewa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kulizindua Bunge hilo la 12 mnamo majira ya asubuhi hapo kesho Ijumaa. Kwa kawaida Mkutano wa Kwanza wa Bunge jipya kama huo huwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analihutubia Bunge kwa maana ya kuweka dira kwenye Serikali yake kwa miaka mitano inayokuja na utekelezaji wa Ilani kadri anavyoona inafaa. Shughuli hiyo ya uzinduzi wa Bunge itatangu...
Wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu.
Kitaifa

Wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu.

  Na.Mwandishi Wetu Dodoma   SPIKA wa Bunge la 12 Job Ndugai amesema wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa miaka mitano mingine (2020-2025) kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge sawa na asilimia 100. “Kura zote zilizopigwa ni 350 hakuna iliyoharibika, hakuna kura ya hapana. Kura zote 350 zimemthibitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, kwa hiyo ndugu wabunge Mheshimiwa Majaliwa amethibitishwa na Bunge hili kuwa Waziri Mkuu kwa kura 350 sawa na asilimia 100.” Spika Ndugai ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 12, 2020) Bungeni jijini Dodoma baada ya kupokea jina la Waziri Mkuu lililowasilishwa bungeni na Mpambe wa Rais na kisha wabunge kupiga kura kwa ajili ya kulithibit...
SOS yakabidhi  chakula kwa wanafunzi.
Kitaifa

SOS yakabidhi chakula kwa wanafunzi.

SHIRIKA la SOS Kisiwani Pemba limekabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi Milioni 1,616,000/=, kwa uongozi wa skuli ya Msingi na sekondari Vitongoji Wilaya ya Chake Chake, kwa ajili ya wanafunzi wanaoishi katika kambi maalumu ya kujiandaa na mitihani yao mwaka huu. Msaada huo kwa skuli ya Msingi Vitongoji ni Mchele kilo 200, sukari kilo 50, maharage kilo 60, unga wa ngano kilo 50, mafuta ya kupikia lita 20, sabuni ya kufulia kilo 15 na Rimu za box za karatasi box 3 vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki 773,000/=. Kwa upande wa skuli ya Sekondari Vitongoji vitu walivyokabidhiwa ni mchele kilo 250, sukari kilo 50, maharage kilo 60, unga wa ngano kilo 50, mafuta ya kula lita 20, sabuni ya unga kilo 15 na Rim box tatu za Karatasi vitu vyote vikiwa na tahamani ya Sh...
Dk. Hussein Mwinyi  azindua  Baraza la Kumi la Wawakilishi
Kitaifa

Dk. Hussein Mwinyi azindua Baraza la Kumi la Wawakilishi

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali  Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane itawekeza kwenye michezo katika kuibua, kuelea na kuendeleza vipaji vya vijana. Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi hafla iliyofanyika huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje kidogo ya Jiji la Zanzibar. Katika hotuba yake hiyo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa katika hatua hiyo ya kuekeza kwenye michezo itakwenda sambamba na kukaa na wadau wa soka kutafuta jawabu la kuamsha msisimko wa ligi ya Zanzibar. “Wakati nakua timu za Zanzibar za Small Simba, Malindi, Mlandege na KMKM zilikuwa ni timu zenye sifa na kuchachafya timu za Bara na zile z...