Wednesday, September 22
WACHEZAJI SIMBA WAPIMWA AFYA YA MAGONJWA YA MOYO JKCI KWA AJILI YA LIGI KUU NA MASHINDANO YA KIMATAIFA
afya, Michezo

WACHEZAJI SIMBA WAPIMWA AFYA YA MAGONJWA YA MOYO JKCI KWA AJILI YA LIGI KUU NA MASHINDANO YA KIMATAIFA

Radiografa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Indrisa Juma akimpima X-ray ya kifua ili kuchunguza moyo na mapafu mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Joash Onyango wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Taddeo Lwanga wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya li...
afya, Kitaifa

Awamu ya pili ya mradi wa uimarishaji wa mfumo wa maji machafu wazinduliwa.

NA ABDI SULEIMAN. KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar, Dr Omar Dadi Shajak amewataka wasimamizi wa mradi wa uimarishaji wa mfumo wa maji machafu Msingini Chake chake, kuhakikisha unatekelezwa kwa viwango na ufanisi ili kufanya kazi kama ilivyokusudiwa. Alisema ili utekelezaji wake uweze kuwa na viwango na ufanisi, lazima mashirikiano ya pamoja yawepo kwa wasimamizi wa mradi huo pamoja na watumiaji wake Dr Shajak aliyaeleza hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa uimarishaji wa mfumo wa maji machafu wa awamu ya pili wa Msingini Chake chake Pemba, hafla iliyofanyika wesha nje kidogo ya mji wa Chake Chake. Aidha alisema kukamilika kwa mradi huo kutazidi kuimarisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira ya bahari, ambayo ndo tegemeo la uchumi wa nchi kufi...
MKURUGENZI Mkuu  TASAC awataka wamiliki wa vyombo vidogo vidogo vya baharini kufuata sheria na kanuni za usajili wake.
Kitaifa, Sheria

MKURUGENZI Mkuu TASAC awataka wamiliki wa vyombo vidogo vidogo vya baharini kufuata sheria na kanuni za usajili wake.

NA ABDI SULEIMAN. MKURUGENZI Mkuu wa wakala wa shirika la meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge, amewataka wamiliki wa vyombo vidogo vidogo vya baharini, wanapaswa kutambua kuwa vyombo hivyo haviruhusiwi kupakia abiria na badala yake kufuata sheria na kanuni za usajili wake. Alisema vyombo hivyo sio sahihi wa kupakia kupakia abiria, kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na kanuni ili kunusuru maisha ya watu na mali zao. Mkurugenzi Kaimu aliyaeleza hayo wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wa pamoja baina ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi SMT na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi SMZ . Alisema vimbo vidogo vidigo sio sahihi kupakia abiria, hivyo wamiliki wanapaswa kutambua kuwa kufanya hivyo...
Makatibu wakuu wanena.
Kitaifa

Makatibu wakuu wanena.

  NA ABDI SULEIMAN. WATENDAJI kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesema kuwa watahakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika kushajihisha waqwekezaji kuekeza katika maeneo Uhuru ya Uwekezaji Micheweni. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi) wa SMT Gabriel Migire, wakati alipokua akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi SMT na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi SMZ, kilichofanyika nje kidogo ya mjini Chake Chake. Alisema Kisiwa cha Pemba kimekua na maeneo mazuri ya uwekezaji, hivyo watahakikisha wanashajihisha wawekezaji kuja kuekeza katika eneo hilo, kwa ajili ya maendeleo ya Kisiwa cha Pemba. “Sisi tutakuwa mab...