Monday, January 17
TIMU ya Vijana Wilaya ya Chake Mapinduzi CUP yapigwa jeki.
Michezo

TIMU ya Vijana Wilaya ya Chake Mapinduzi CUP yapigwa jeki.

NA ABDI SULEIMAN. TIMU ya Vijana Wilaya ya Chake Chake Mapinduzi CUP, imekabidhiwa vifaa mbali mbali vya michezo pamoja na vyakula kwa ajili ya kambi ikiwa ni maandalizi ya safari ya kwenda Unguja Wikii. Vifaa hivyo walivyokabidhiwa ni mchele, mafuta ya kupikia, sukari, maharage, Trak Suti na jezi kutoka kwa viongozi wa wilaya hiyo. Akikabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, aliwataka wanamichezo hao kuendeleza nidhamu walionayo wakati wote wa mashindano hayo. Alisema nidhamu ni moja ya ushindi kwani zipo timu zinapatiwa zawadi kuwa timu bora yenye nidhamu, huku akiwataka kuhakikisha wanarudi na ubingwa wa mashindano hayo. ”Michezo sio burudani tu kwa sasa bali michezo ni ajira pia kwa wachezaji, vizuri kuongeza nguvu na juhudi ili kufikia m...
Makamu wa Pili wa Rais Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Kitaifa

Makamu wa Pili wa Rais Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar

  Na Othman Khamis , OMPR Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla  alisema Tangazo la Elimu Bila ya Malipo lililotolewa mara tu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 lilikuwa na maana ya kuongeza fursa za kupata Elimu iliyo bora kwa wote. Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema hayo wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Donge Mkoa Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964. Alisema Elimu bora na ya kiwango ndio inayomuwezesha Mwanaadamu hasa Watoto wa Taifa hili kukabiliana vyema na changamoto mbali mbali watakazokuwa wakipambana nazo katika maisha yao, Wazazi na hata Taifa kwa ujumla. Mh. Hemed alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanz...
Wakuu wa Wilaya wa Unguja na Pemba Watakiwa Kwenda Kuwatumikia Wananchi na Kuimarisha Ulinzi Katika Wilaya Zao – Dk Mwinyi
Kitaifa

Wakuu wa Wilaya wa Unguja na Pemba Watakiwa Kwenda Kuwatumikia Wananchi na Kuimarisha Ulinzi Katika Wilaya Zao – Dk Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wakuu wapya wa Wilaya  walioapishwa kuhakikisha kunakuwepo ulinzi na usalama wa kutosha katika Wilaya zao. Dk. Mwinyi ametoa maelekezo hayo wakati alipowaapisha Wakuu wa Wilaya kumi (10) za Unguja na Pemba, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar. Disemba 28, mwaka 2020 Rais Dk. Mwinyi alifanya mabadiliko ya Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 11 za Zanzibar kwa kumteua Marina Joel Thomas kuwa Mkuu wa Wilaya Kati Unguja, Issa Juma Ali (Mkoani), Hamida Mussa Khamis (Magharibi ‘B’) na CDR Mohamed Mussa Seif kuwa Mkuu wa Wilaya Micheweni Pemba. Wengine walioteuliwa na kuapishwa ni Rashid Simai Msaraka (Mjini Unguja), Sadifa Juma Khamis (Kaskazini ‘A’), Aboud Hassan Mwinyi (Kaskazini ‘B’), Rashid Makame...
Kitaifa

Wananchi wampongeza Mbunge wao.

  NA ABDI SULEIMAN. WANANCHI wa shehia kiuyu kigongoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wamempongeza mbunge wa jimbo la Kojani kwa kuendelea kuwatatulia matatizo mbali mbali yanayowakabili katika shehia yao. Wananchi hao walisema kuwa kwa mda mrefu walikuwa na tatizo la  maji katika kijiji cha fimbo, ambapo tataizo hilo kwa sasa limetatuliwa baada ya mbunge huyo kuwapatia mpira mpya wamaji na kuufukia. “Hapa maji ilikuwa yanamwagika kwa wingi sana, hata majumbani hayafiki yanaishia hapa barabarani kutokana na kupasuaka kwa hili boba, tulishalitengeneza zaidi ya mara mbili lakini bado, sasa mbunge ametusaidia na maji yanafika”walisema. Yussuf Faki Hamad kutoka kijiji cha Chwakani shehia ya Kiuyu Kigongoni, alimshukuru mbunge huyo kwa kupatia fedha za kueze...
RC MAPINDUZI ndio kila kitu Zanzibar.
Kitaifa

RC MAPINDUZI ndio kila kitu Zanzibar.

  NA ABDI SULEIMAN. MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, amewataka wazazi kuwaleza vijana wao juu ya dhamira na madhumuni ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, pamoja na kuwajenga katika vijana kuwa wazalendo. Alisema Mapinduzi matukufu ya 1964 ndio kila kitu kwa wananchi wa Zanzibar, hivyo wazazi wanapaswa kuwafundisha vijana wao juu ya dhamira ya mapinduzi hayo pamoja na kuifahamu falsafa nzima ya Mapinduzi. Mkuu huyo wa Mkoa aliyaeleza hayo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ufanyaji wa usafi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Chake Chake, ikiwa ni shamra shamara za miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Alisema lazima watoto wajengwe katika suala zima la kuwa wazalendo wa Mapinduzi nan chi yao pia, ikiwemo suala la kudumisha amani pamoja na kutek...