Monday, January 17
CUF yazindua kampeni Pemba.
Kitaifa, Siasa

CUF yazindua kampeni Pemba.

MGOMBE Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa CUF inaomba kura kwa sababu chama hicho katika vyama vyote ndicho kinachosimamia haki sawa kwa wananchi wote. Alisema katika jambo ambalo CUF walifanikiwa kulipata Zanzibar katika mapambano ya kisiasa, ni katiba inayozungumzia uwepo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa. Profesa aliyaeleza hayo wakati wa ufunguzi wa Kampeni za chama hicho, zilizofanyika katika uwanja wa michezo Tibirinzi mjini Chake Chake Pemba, huku zikihudhuriwa na wanachama na wananchi wa chama hicho. Alisema CUF imekuwa ni waasisi wamaridhiano, waasisi wa mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ambayo imepelekea kuwepo kwa serikali ya umoja wa Kitaifa. “Ndugu zangu nyote mnakumbuka tuliingia ka...
DK. Shein aweka jiwe la msingi Pemba.
Biashara, Kitaifa

DK. Shein aweka jiwe la msingi Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amesema kuwa sula la viwanda kwa Zanzibar ni suala la miaka mingi sana, kabla ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 na baada ya Mapinduzi, ikiwemo viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa. Alisema viwanda hivyo vilikuwa vya sabuni, usumba, mafuta ya nazi, viwanda vya soda, maziwa, Mapinduzi ya mwaka 1964 ndio yaliobadili maendeleo hayo. Dk.Shein aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba, mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kusarifia Mwani uliokwenda sambamba na Uzinduzi wa eneo la Viwanda Chamanangwe II Mkoa wa Kaskazini Pemba. “Zanzibar ilikuwa imenawiri kwa viwanda vidogo vidogo, ikiwemo viwanda vya maziwa, mterekta, soda, kiwanda c...
Ni vizuri kufuga wanyama ila……………
Biashara, Kitaifa, Makala

Ni vizuri kufuga wanyama ila……………

KATIKA miaka ya hivi karibuni Dunia imekuwa ikishuhudia magonjwa mbali mbali kujitokeza, yapo yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa Duniani, pia yapo yanayotokana na wanyama moja kwa moja. Katika magonjwa hayo yapo yanayotibika kwa Chanjo, pia yapo ambayo hadi sasa chanjo yake imeshindikana kupatikana, zaidi ya kutumia dawa ili kupunguza nguvu ya virusi vya ugonjwa huo. Zoonosis ni ugonjwa ambao huambukizwa kutoka kwa wanyama wenye utu wa mgongo kwenda kwa mwanaadamu, ambapo kuna aina zaidi ya 200 ya magonjwa hayo, Zoonoses inajumuisha asilimia kubwa ya magonjwa mapya na yaliyopo kwa wanaadamu. Vimeelea vya Zoonosis vinaweza kuwa ni baktiria, Virusi au vimelea vyengine, yapo magonjwa yanayoweza kutibika kwa chanjo kwa 100%, ikiwemo kichaa cha mbwa. Kampeni ya elimu ya ...
Maalim Seif kukuza pato la mwani akiingia Ikulu tu
Kitaifa, Siasa

Maalim Seif kukuza pato la mwani akiingia Ikulu tu

MGOMBEA  wa urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha ACT- Wazalendo maalim Seif Sharif Hamad, amesema endapo wananchi wa Zanzibar watamchaguwa na kumuweka madarakani,  atahakikisha wakulima wa mwani wanapata faida kwa kuweka bei nzuri ambayo itakidhi machungu ya kilimo hicho. Maalim Seif aliyaeleza hayo huko Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba, wakati akizungumza na wakulima wa mwani pamoja na wavuvi wa eneo hilo, katika ziara yake kisiwani humo. Alieleza kuwa, wanunuzi wa mwani  wanakuwa wanawadhulumu  wakulima kwa kununua zao hilo kwa bei ya chini ya shilingi 600 kwa kilo moja. “Tukingia madarakani nitahakikisha Serikali yangu inawahudumia wakulima wa mwani, kwa kuwapatia vyombo ambavyo vitafika maji makubwa, ili waweze kulima mwani bora wa Cotonee ambao unabei kubwa katika...
Wanawake wanaweza, watizameni kwa jicho la maendeleo
Biashara, Kitaifa, Siasa, Wanawake & Watoto

Wanawake wanaweza, watizameni kwa jicho la maendeleo

Imeandikwa na Amina Ahmed – Pemba Walio Wengi wanafikiria ya kuwa mwanamke hawezi  kusimama  na kugombea nafasi  ya uwongozi katika jimbo iwe ya Uwakilishi, Ubunge Udiwani na nyadhifa nyengine lakini, Kuelekea  Uchaguzi Mkuu  October 28 mwaka huu 2020 baadhi ya wanawake wameweza kuonesha ujasiri wa kugombea nafasi za uongozi  majimboni  licha ya awali  kukabiliwa na changamoto ya virusi vya korona huku ikiwa ni mara ya kwanza kuingia katika mchakato wa kugombea  . Leo katika makala hii  maalum ya wanawake na uongozi  tutamuangalia  mjasiriamali mwanamke  alieamua kujitosa katika  Nyanja ya kisiasa na kufanikiwa   kugombea nafasi ya ubunge  katika jimbo la chake chake  Mkoa wa kusini Pemba kupitia chama cha cha wakulima  AAFP. Ni Fatma Doto Shauri Mkaazi wa Madungu chake chak...