Milele yakabidhi vifaa kwa Hospitali ya Chake Chake.
TAASISI ya Milele Zanzibar Foundation Pemba, imekabidhi mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuwaji na nguo(auto clave), pamoja na mashine ya kufulia nguo vyote vikiwa na tahamani ya shilingi Milioni 14 kwa uongozi wa Hospitali ya Chake Chake.
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni mashine ya auto clave yenye thamani ya shilingi Milioni 12 na mashine ya kufulia nguo yenye thamani Milioni mbili.
Akuzungumza katika hafla ya kukabidhi mashine hizo, kwa uongozi wa hospitali ya Chake Chake, mratib wa Taasisi ya Milele Ofisi ya Pemba Abdalla Said Abdalla, alisema taasisi hiyo imo katika harakati za kusaidia jamii katika kuwakomboa na umasikini.
Alisema Milele imekuwa imejikita katika kusaidia sehemu tafauti ikiwemo elimu, Afya, Uchumi, ili kuwahikisha wananchi wananufaika na uondokana na...