Wawakilishi wateuliwa wanena.
WAWAKILISHI wateule wa Majimbo Mbali Mbali Mkoa wa Kusini Pemba, wamesema kuwa sasa kazi iliyombele yao ni kuhakikisha wanatimiza kwa vitendo ahadi zote walizozitoa katika mikutano ya kampeni wakati wakiomba kura kwa wananchi.
Wawakilishi hao amboa wameshinda katika majimbo yao ya uchaguzi na kuthibitishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC na kupatiwa vyeti vya uthibitisho huo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baada ya kumailiza kwa matokeo ya uchaguzi, walisema watahakikisha wanatekeleza yote walioyaahidi kwa wananchi wakati wakiwaomba kura.
Mwakilishi mteule wa jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, Suleiman Massoud Makame alisema ushindi alioupata umetokana na kazi nzuri, iliyoifanya ya kuwaelimisha wananchi kuchagua CCM wakati wa kampeni.
Aliwataka wan...