Friday, April 23

VIDEO: SEREKALI IMEGUSWA NA MSIBA WA MZEE SALUM MKWECHE” MHE. HEMED MAKAMU WA PILI WA PILI WA RAIS

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali imeguswa na kufikia uamuzi wa kuungana na wanafamilia pamoja na Wanamichezo wote kwenye msiba wa Viterani wa Michezo Nchini Mzee Salum Mkweche.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo alipofika nyumbani kwa mwanamichezo huyo Kokoni Mjini Zanzibar, kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu huyo, kwa kuondokewa na mzee wao.
Akitoa salamu za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi, Mheshimiwa Hemed amesema  Dr Mwinyi anawapa pole watoto wa marehemu na wanafamilia hao, na kuwa anatambua mchango wa Mwanamichezo huyo wa zamani nchini, na kuwa yupo pamoja na Familia hiyo katika kipindi hichi kigumu.
Kwa upande wao Wanafamilia hao wakiwasilishwa na Mmoja wa  Mtoto wa Marehemu Bwana Nassor Salum Mkweche amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa, Marehemu alikuwa ni Mwanamichezo aliyesifika kwa kipaji cha kipekee ambacho ndicho kilichompatia hadhi na kuwa maarufu katika michezo.
Marehemu Viterani wa Michezo Nchini Mzee Salum Mkweche amezikwa Jumapili ya tarehe 31 Januari katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Aamin.
ANGALIA VIDEO