Waandishi wa habari habari wametakiwa kufikiria mbinu au njia zitakazotumika kuleta amani nchini.

 

WAANDISHI wa habari wametakiwa kufikiria mbinu au njia mbali mbali ambazo watazitumia kuleta amani nchini, pamoja na kumaliza machafuko yanayoendelea duniani kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Hayo yameelezwa na aliyekua Afisa Mdhamini ya Habari utalii na Mambo ya Kale Pemba Khatib Juma Mjaja, wakati alipokua akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Pemba, juu ya kushajihisha masuala ya amani na mijadala ya kijamii inayohusiana na upatikanaji wa haki baada ya uchaguzi Mkuu mkutano ulifanyika Mjini Chake Chake.

Alisema kalamu za waandishi wa habari zinafika mbali iwapo wataweza kuzitumia, kwa kuandika taarifa mbali mbali zinazohusiana na amani na kuzisambaza katika miatandao ya Kijamii.

Alisema tokea mwaka 2010 dunia imeingia katika machafuko makubwa, machafuko ambayo bado yanazidi kuendelea hali inayoifanya dunia kutokuwa salama.

“Iwapo mitandao ya kijamii itatumika vizuri katika suala la kuhamasisha amani, badi Dunia itarudi chini na machafuko yote kuzuilika na amani iyendelee kudumua, iwapo waandishi wa habari watakuwa tayari kuelimisha umma juu ya umuhimu wa amani”alisema.

Alifahamisha kuwa zaidi ya watu Milioni 68 wanakimbia nchi zao tokea kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, huku akisema kuwa vita sio kitu kizuri kwani kinamuathiri kila mmtu.

“Hetu tuangalieni kipindi cha Corona kila mtoto hata nje alikuwa hatoki, jee vita hata ibada itashindwa kufanyika kwa amanai, lakini sasa kila mtu anatembea anavotaka na kufanya mambo yake”alisema.

Majaja alisema inakadiriwa ifikapo 2030 nusu ya watu duniani kote watakuwa wanaishi katika nchi zenye migogoro, hivyo aliwataka wananchi nchini kuendelea kudumisha kwa kuhakiisha wanakua kitu kimoja, pamoja na kuzidisha mshikamano.

Hata hivyo alisema masuala ya utanzaji wa amani yanatakiwa kuwemo katika mitaala ya elimu ili watoto waweze kufundishwa skulini, hadi atakapomaliza masomo anakuwa kijana mzuri wakuelimisha wenzake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kalbu ya Waandishi wa habari Kisiwani Pemba (Pemba Press Club) Bakar Mussa Juma, aliwataka waandishi wahabari kuisaidia Serikali iliyopo madarakani ya Umoja wa Kitaifa, katika kuwahamaisha wananchi juu ya suala zima la amani na utulivu uliopo uwendelee kudumu.

Alisema waandishi wa habari ni watu mashuhuri katika kuelimisha jamii na kuyatangaza maendeleo yaliyofanywa na serikali, hivyo wanapaswa kutumia kalamu zao katika kulendelea kuelisha juu ya masuala mazina ya kudumisha amani nchini.

Hata hivyo nao waandishi wa habari kiswani Pemba wameipongeza Pemba Press Club kwa kuwapatia mafunzo hayo pamoja na kuwakumbusha wajibu wao katikla kuendeleza amani iliyopo nchini.

Mafunzo hayo ya siku moja yametolewa na Klabu ya waandishi wa Habari Kisiwani Pemba (Pemba Press Club) kwa kushirikiana na Internews.

EMAIL:abdisuleiman33@gmail.com