PPC YAFANYA MKUTANO MKUU MAALUM NA KUPITISHA MAAZIMIO 10 YA MKUTANO MKUU MAALUM WA UTPC.

NA ABDI SULEIMAN.

MWENYEKITI Mstaafu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) Said Mohamed Ali, amewakumbusha wanachama wa klabu hiyo wasikubali kuandika habari kwa utashi wa mtu au kwa kupewa maelekezo, badala yake kufuata kanuni na maadili ya taaluma yao.

Alisema waandishi wa habari ni watu mashuhuri duniani, hivyo wanapaswa kufuata taaluma kwa kuandika  habari zao, kwani bado jamii inawahitaji na wanapaswa akutumia lugha nzuri kwenye habari.

Mwenyekiti huyo Mstaafu aliyaeleza hayo wakati akifungua mkutano mkuu  malumu wa  wanachama wa PPC, kwa ajili ya kupitia maazimio yaliyotolewa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UTPC, mkutano uliofanyika Ukumbi wa Mkataba kuu ya Chake Chake.

“Lazima tubadilike katika kuandika habari zetu na tutumie vizuri kalamu zetu kwa kufuata maadili, jamii na nchi inatutegemea na tujue watu wahatosita kutumia habari yako kwa kile wanachokiamini,”alisema.

Aidha aliwasihi waandishi kutokuwa chanzo cha kuleta migongano na kutokua na maelewano, bali wanapaswa kuwa chanzo cha kuleta amani katika nchi na jamii kuwa na maelewano mazuri.

Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo mstaafu, alisema wakati umefika wa kubadilika pale rasilimali za nchi zinapotumiwa vibaya, ni busara waandishi kutumia lugha nzuri katika kukemea matumizi mabaya ya rasilimali hizo.

Hata hivyo aliwataka waandishi kwenda sambamba na mabadiliko ya dunia katika matumizi ya mitandao ya kijamii, kwa kuweka habari na picha zao zenye kueleimisha jamii na zenye manufaa kwa umma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa PPC Bakari Mussa Juma, akiwasilisha Mwelekeo wa UTPC, alisema wafadhili wanataka Press Club ziwe na mabadiliko na ziweze kujisimamia, wafadhili wapo tayari kufanya kazi na klabu hata sita ambavyo vipo tayari kufanya kazi.

Alisema waandishi wanapaswa kuwa tayari kufanya kazi ili wafadhili waweze kuleta walichokusudia, pamoja na kutumia mitandao ya kijamii vizuri kama ilivyo kwa Habari Portal.

Akiwasilisha mwelekeo wa PPC Katibu wa Klabu hiyo Ali Mbarouk Omar, aliwataka wanachama wa PPC kujiongeza kitaaluma na wasitosheke na elimu walionayo, kuendeleza umoja na mshikamano uliopo, kuongezea mashirikianao na taasisi nyengine, kuwasisitiza wanachama kulipa ada ya klabu.

Naye Msaidizi Katibu wa PPC Mchanga Haroub Shehe, akiwasilisha Ripoti fupi ya Mwaka 2022 ya Pemba Press Club ambayo ni pamona na wanachama wapya, mafunzo waliopatiwa, miradi iliyotekelezwa, misaada iliyotolewa na wadau na changamoto na mafanikio.

Wakichangia katika mkutano huo, Said Mohamed alisema kila mwandishi anapaswa kila wiki kutuma habari japo mbili kwa wahariri wa mtandao wa Habari Portal ili kuchapishwa.

Asha Mussa aliwasihi wanachama kufahamu kuwa, bila ya kulipa ada ya mwaka kwa mwanachama klabu haitoweza kwenda mbele, badala yake inaweza kupoteza hata mwelekeo.

Aidha alishauri kutafutwa kwa wataalamu watakaoweza kuandika miradi kwa ajili ya klabu, kwani wanachama ndio watekelezaji wakubwa wamiradi hiyo inapopatikana.

Hata hivyo wanachama wa Mkutano maalumu huo, wamepitisha maazimio mbali mbali ya Mkutamno Mkuu wa UTPC uliofanyika hivi karibuni.

MWISHO