Milele Zanzibar Foundation yatoa msaada kwa wanafunzi wa Skuli ya Utaani na Chasasa.
NA HANIFA SALIM.
TAASISI ya Milele Zanzibar Foundation, imetoa msaada wa vifaa kwa manusura waliopata na janga la moto katika skuli ya sekondari Utaani na Chasasa Wete vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 20.
Msaada uliotolewa kwa wanafunzi hao ni mikoba 404, kanga 481, viatu 500 na wino nne za fotokopi kufuatia kwa janga la moto liliopelekea kuungua kwa nyumba wanayolala wanafunzi wa kike (dahalia) mwezi machi mwaka huu.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa taasisi ya milele Zanzibar Foundation Pemba Abdalla Said Abdalla alisema, fedha hizo ambazo zimetolewa ni ahadi walioiweka mara tu baada ya kutokea janga la moto kwenye skuli hiyo.
Alisema, hatua zinazochukuliwa na milele ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dk...