Rais wa UTPC atua PPC

Viongozi wa PPC wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa UTPC Deogratius Raymond Nsokolo( Rais wa pili Kulia).

Viongozi wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini wametakiwa  kuwa na mashirikiano ya kutosha na wanachama wa vilabu hivyo ili waweze kutumikia wananchi  kwa ufanisi zaidi.

Wito huo umetolewa na Rais wa  Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzinia   (UTPC ) Deogratias  Nsokolo wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Klabu ya Waandishi wa habari Kisiwani Pemba ( Pemba Press Club)  huko ofisini kwao Misufini Chake Chake  Pemba .

Amesema waandishi wa habari   wanajukumu la kusaidia kupaza sauti za wasio na sauti ili waweze kusikika  na kuchukuliwa hatua kwa changamoto zao zinazowakabili hivyo bila ya kuwepo mashirikiano ya dhati kazi hio haiwezi kufanyika ipasavyo.

Amesema wananchi hasa wa vijijini wamekabiliwa  na changamoto nyingi hivyo waandishi wa habri ndio wenye uwezo wa kuzifichua  na kuweza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Rais huyo amewataka waandishi kufahamu umuhimu wa kazi zao katika jamii huku wakiongeza bidii ya kuwatumikia wananchi  ili kuwasaidia wao na Taifa kwa ujumla.

Amesema UTPC itahakikisha inavisaidia Vilabu vya waandishi wa habari  kadiri hali itakavyo ruhusu ili viweze kumudu kutekeleza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.

Aidha amewaasa viongozi hao kuwa wavumilivu na kustahamiliana ili kusudi kuipeleka mbele klabu yao.

Akizungumzia katika suala la bima ya afya wa wanachama, amesema ni muhimu kuwashajihisha wanachama kukata kwani zitawafaa kwa kupunguza harama za matitabu anapotokezewa na maradhi mbali mbali.

 

“Ndugu viongozi jitahidini kuwashajihisha wanachama kukata bila ya afya kwani ni nzuri kwa maslahi ya afya zao kwani afya ndio kila kitu kwa binaadamu” amesema.

Akizitaja bei za bima amesema kwa mtu mzima ni sh 100,000/= tu  na mtoto ni sh elfu hamsini na mia nne .

Rais huyo wa UTPC ambae alifika kisiwani Pemba kwa ziara ya siku moja ni katika mfululizo wa ziara zake za kuvitembelea vilabu vya waandishi wa habari  nchini na kukutana na  uongozi wa vilabu hivyo ambapo pia kwa PPC imeambatana na uzinduzi wa Uongozi mpya ambao uliingia madarakani tarehe 06/09/2020.