PPC wafanyiwa tathmini ya mapitio ya mradi wa Dumisha Amani Zanzibar.

KLABU ya waandishi wa  habari kisiwani Pemba (PPC) wanatarajia kutekeleza  mradi wa Dumisha Amani Zanzibar utakaojulikana kwa jina la “SAUTI YANGU, AMANI YANGU, HTIMA YANGU”  ambao utakelezwa kwa mashirikiano baina ya Foundation for Civil Society, Search for  Common Ground chini ya ufadhili wa umoja wa nchi za Ulaya (European Union).

 

Ukiwa na dhamira kuu ya kuongeza uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa kudumisha amani na utulivy kutokana na migogoro inayojitokeza hasa wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

 

Hivyo basi watendaji wa foundation na Search wamefika ofisi za PPC kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kujidhihirisha juu ya ufanyaji kazi wa Taasisi pamojana nutoa maelekezo ili kuboresha zaidi.