Monday, May 20

EJAT  imeondosha  makundi 5 ya habari katika mashindano hayo kwa mwaka huu wa 2023.

NA FATMA HAMAD –  DODOMA.

Kamati ya mandalizi ya Tunzo za Umahiri za Wandishi wa habari Tanzania EJAT imeondosha kundi la habari za Sensa, Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini pamoja na habari za Sayansi na Teknolojia katika mashindano hayo kwa mwaka huu wa 2023.

Akizungumza na Wandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali katika mafunzo malumu ya uwandishi wa Habari za haki za binadamu Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi wa Ijati ya mwaka 2023 Kajubi Mukajanga  huko Dodoma Tanzania Bara.

Alisema kamati hiyo imeondosha Tunzo  hizo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kukosekana kwa habari zinazoshindaniwa kwenye kundi hilo.

Aliendelea kusema licha ya kuondolewa kwa makundi hayo Bali kuna makundi mawili mapya yameongezwa ikiwemo Habari za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na habari za Malezi na Makuzi ya Awali ya Mtoto ili kushajiisha ubora wa uandishi wa habari katika maeneo hayo.

Alifahamisha kuwa wandishi wenye Habari  za maeneo hayo yaliotolewa ambao wanaona kazi zao ni nzuri wataziwasilisha kupitia makundi mengine kama vile Uchumi, Biashara, na Fedha, au Elimu, au kundi la Wazima.

Alifafanua kuwa licha ya kamati ya Mandalizi ya EJAT kutoa Tunzo na zawadi kwa washindi, pia MCT hutoa udhamini wa masomo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania Million 3,000,000 kwa mshindi wa jumla ili ajiendeleze kitakuma katika masuala ya uwandishi wa Habari kulingana na mahitaji yake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya wandishi wa habar Tanzania UTPC Kenneth’s Simbaya alisema wandishi wengine handiki Habari zinazo wahusu Watoto, hivyo amewataka wachukue jitihada za makusudi waweze kuziibua kero zinazo wakwaza ili ziweze kujulikana na kuchukuliwa hatua.
Baadhi ya wandishi wa habar walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Lugendo Madege na Meri Laine walisema mafunzo hayo yamewasaidia kujua namba Bora ya kuandaa makala zinazofaa kushindanishwa kwenye Tunzo za EJATI.
Katika kuandaa Tunzo hizo MCT inashirikiana na wadau wengine wa habari wakiwemo Tasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Misa Tan), Wakfu wa vyombo vya habari Tanzania (TMF), Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF), Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Umoja wa Klabu za Wandishi wa habari Tanzania UTPC pamoja na Haki Elimu.