Monday, May 20

TIMU ya wanaume wa Mabadiliko Wilaya ya Mkoani, wameiyomba serikali nyumba ya kurekebisha tabia kwa watoto wanaokinzana na sheria.

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

 

TIMU ya wanaume wa Mabadiliko Wilaya ya Mkoani, wameiyomba serikali kupitia Wizara husika, kuhakikisha ndani ya Kisiwa cha Pemba inajengwa nyumba ya kurekebisha tabia kwa watoto wanaokinzana na sheria.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa timu hiyo, ambae Pia ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria Wilaya ya Mkoani Nassor Hakim, wakati akichangia katika mkutano maalumu, ulioandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na kufanyika ofisi za Mkuu wa Wilaya Mkoani.

Alisema kuwepo kwa nyumba hiyo ingesaidia watoto wanaokinzana na sheria, kwani wangeweza kuweka huko hata akitoka mtoto tayari ameshajifunza tabia njema.

“Mtoto anapofanya kosa saivi anatakiwa kuadabishwa, lakini kwa vile nyumba hiyo unaona wazazi wanalipa wao faini baada ya kosa kufanya mtoto ndio adabu pia zikapungua,”alisema.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema nyumba hiyo kuwepo ni kwa ajili hya watoto, hata wale waliodhalilishwa wanapaswa kuwemo, kwani watapata elimu ya saikolojia na sio kubakia mtaani.

Alisema katika kamati za kutoa elimu akinababa wengi hawapatikani, hivyo kuundwa kwa kamati hiyo kutawafanya wanaume kupata fursa ya wanaume kushirikishwa moja kwa moja.

Nae katibu wa baraza la Vijana shehia ya Mbuguani, Salum Hamad Juma alisema sifa kubwa ya wananchi wa visiwani ni suala la muhali kwa kila jambo.

Alisema muhali huo hauwafikishi sehemu yoyote, kwani matukio ya udhalilishaji yanadhidi kuongezeka baada ya kupungua kutokana na mikakati mbali mbali inayochukuliwa.

Kwa upande wake Mohamed Said Mohamed, alisema suala la udhalilishaji bado serikali haijataka kulichukulia hatua, kwani inapotaka jambo lake hakuna wa kulizuwia.

Mapema msaidizi Afisa Maendeleo ya Wanawake Tahadudi Juma Othaman, aliitaka timu za Wanaume wa mabadiliko Wilaya ya Mkoani, kushirikiana na akina mama ili kufikia mbele malengo ya kuundwa kwa timu hizo.

“Kuwepo kwa watu mchanganyiko kwenye timu hii ni jambo zuri na itasaidia katika utoaji wa elimu kwa jamii, sasa wapo watu wataweza kuwaamini wanaume wenzao wakiwemo viongozi wa dini,”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Ali Wadi, alisema kikosi hicho mchanganyiko cha wanaume wa mabadiliko, kitaweza kutoa elimu kwa jamii juu ya kupiga vita vitendo vya udhalilishaji katika maneo mbao mbali.

Alisema timu hiyo itaweza kuwashirikisha watendaji kutoka taasisi mbali mbali za serikali, binafsi wote leo lao ni mojmoja tu kusaidia kuondosha vitendo vya udhalilishaji.

Nae Mkuu Divisheni ya Maendeleo ya Watoto na mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji Mohamed Jabir, alisema lengo la kikao hicho ni uanzishwaji wa timu ya wanaume wa mabadiliko katika kuoinga vitendo vya utakili na udhalilishaji wakijinsia.

Alisema timu hiyo itaweza kutoa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa wanaume, kwa sababu wanaume taarifa zao hazipatikani sasa wataweza kuibua matukio na kuyafikisha katika vyombo vya sheria.

MWISHO