JUKWAA LA PILI LA MSAADA WA KISHERIA ZANZIBAR LAZAA MAAZIMIO 16 KUELEKEA 2023
JUKWAA LA PILI LA MSAADA WA KISHERIA ZANZIBAR 2022
Laibua maazimio 16 yenye shabaha ya uimarishaji utoaji msaada wa kisheria
LSF yaahidi makubwa, Mkurugenzi Hanifa aupiga mwingi
NA HAJI NASSOR, PEMBA
DISEMBA 13 na 14 mwaka 2022, ilikuwa ni siku adhimu na adimu, zilizofanyika jukwaa la pili la msaada wa kisheria Zanzibar.
NINI MAANA YA JUKWAA?
Ni mkutano, mjadala, kongamano la wazi linalowakutanisha wadau wa haki jinai, kujadili, kubadilishana uwezo na kukosoana, kwa njia amani.
Maana kupitia jukwaa hilo, linalowakutanisha wadau zaidi ya 200 kutoka Unguja na Pemba, huandaliwa na wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, chini ya Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria.
Jukwaa hilo, liliwakutanisha watoa msaada wa kisheria, wasaidizi wa sheria, mahakimu, waendesha ...